JIFUNZE KWA YAKOBO_Sehemu ya Tatu

Na Denis Mushi

Kama tulivyo angalia kwenye sehemu Ya kwanza na ya pili juu ya maisha ya Yakobo, hapa natamani tuone sehemu hii ya tatu ya ENEO LA KIUCHUMI
BIBLIA INASEMA katika 3Yohana 1:2
" Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako kama vile roho yako ifanikiwavyo "
Huu mstari unamaana pana kidogo tukiyachukulia maisha ya Yakobo Mungu alihakikisha maisha yake yakiroho yanafanikiwa kwanza ndipo ayafanikishe na Ya mwili ..
"ILI UFANIKIWE KIMWILI NI LAZIMA UANZE KUFANIKIWA ROHONI"
Mara nyingi Tunakuwa tukisikia mahubirii na mafundisho mengi kuhusu kufanikiwa kiuchumi LAKINI Hakuna mafanikio yoyote yakiuchumi yanayoweza kutokea kwenye maisha yako kama huna bidii ya kutafuta hayo mafanikio.. HAKUNA MAFANIKIO YA PAPO KWA HAPO LAZIMA UWE NA BIDII YA KUYATAFUTA
ANACHOKIFANYA MUNGU NI KUKUPA NGUVU YA KUFIKIA HUO UTAJIRI
Biblia inaweka wazi kuwa Yakobo licha ya kuwa aliishi kwa ndugu yako lakini alikuwa akifanya kazi tena ya kulipwa mshahara
Ingawa akifanya kazi Kwa mjomba wake lakini alidhulumiwa mshahara wake mara kumi
Anasema hivi "" Miaka hii 20 nimekaa nyumbani kwako nilikutumikia miaka kumi na minne Kwa binti zako wawili na miaka sita Kwa wanyama wako NAWE UMEUBADILI MSHAHARA WANGU MARA KUMI ""
Maana yake kama alikuwa analipwa kila mwezi ni kuwa kuna mwaka ambao miezi kumi hakulipwa kabisa mshahara wake...
Licha ya kutokulipwa mshahara wake hakuwahi kumuibia mjomba wake wala kukaa tamaa ya kuacha kufanya kazi yake..
Haikuwa Rahisi Kwa Yakobo kufanikiwa kiuchumi kama HAJAPATA ndoto angalia maneno haya anayoyasema
MWANZO 31:40 " HII ILIKUWA HALI YANGU; MCHANA JUA LILINIPATA NA BARIDI USIKU , USINGIZI UKANITOKA MACHONI MWANGU ..
Mungu alimtengenezea Yakobo ufahamu juu ya eneo la uchumi..Licha ya kuwa alitumika miaka 14 Kwa ajili ya wake zake wawili lakini pia ajiongeze miaka mingine 6 kuhakikisha anao uwezo Wa kiuchumi Kwa ajili ya kuitunza familia yake
MAMBO MUHIMU YA KUJIFUNZA HAPA KWA YAKOBO
1: Mafanikio yoyote ya kiuchumi hayawezi kuja pasipo kulishughulika na kuanza Kwa kufanya mambo madogo madogo ..Usisubiri mambo makubwa anza na hilo hilo lililolidogo Mungu ataliongeza like kubwa
2: Uhusiano wako na Mungu ukiwa mzuri Mungu anaachilia wazo ndani yako litakalo kusaidia kukua kiuchumi
3: Yakobo alihakikisha anafanyia kazi kila wazo ambalo Mungu alikuwa ameweka ndani yake ili limsaidie kukua kiuchumi . MWANZO 29:37-43
4: Anachokifanya Mungu sio kukupa Mali nyingi wala utajiri mwingi ILA ANAKUPA WAZO/ AKILI AMBAYO KAMA UTAIFANYIA KAZI NDIPO UTAFANIKIWA KIUCHUMI
5: Siyo kila wazo yakiuchumi linalokuja ndani yako unalichukulia kirahisi tu mengine ndio yatakayo kutoa hakikisha unashughulikia wazo lolote la kiuchumi linalokuja ndani yako
6: Kamwe usitafute njia Rahisi za kufanikiwa kwani zinaweza kuwa na madhara Kwako na hata familia yako ..kuwa mvumilivu na kumwamini Mungu nae atakuinua Kwa wakati wake.
Mwisho.....
Mungu akubariki mno Nakutamkia kufanikiwa Rohoni na mwilini katika jina la Yesu
Previous
Next Post »