Judith Mbilinyi_Wewe uko Hapa (New Album)


Baada ya kumalizika kwa Albamu yake ya kwanza iliyokwenda kwa jina la "Wamekosa nini?", mwimbaji wa nyimbo za injili Judith Mbilinyi anakuja na ujio mpya kabisa wa Albamu nyingine ambayo kwa hakika itakuwa inavutia. Awali mwimbaji huyo alikuwa anawaza kufanya "live recording" amekwama kwa sababu ya kukosekana kwa fedha za kununua vifaa.
  Akiongea na Sound Of Worship, Judith Mbilinyi amesema haya:-
          "Kwenye albamu yangu hii mpya huenda nikamshirikisha mwimbaji wa nyimbo za injili Angel Benard. Pia nina hamu na ni shauku yangu kwamba wana Sound Of worship wangeshiriki katika nyimbo zangu."



  Aliongeza kwamba anaendelea kujifua katika kutumia vyombo vya muziki ambapo kwasasa anaendelea na kujifunza kupiga gitaa. Anasema mara ya kwanza kutumia ilikuwa vigumu sana maana alitumia nguvu sana, mpaka vidole kuuma.






Facebook | | Instagram | YouTube
Email: judithmbilinyi@gmail.com
Tel: +255 762 372 408

Mwachie maoni yako hapa



Previous
Next Post »