Tatizo sio kwamba hatuwezi kufanya ila tatizo ni kwamba hatutaki kukubali udhaifu wetu nã kuwaruhusu tu wale wanaoonekana kuwa hodari katika hilo wakalifanya hilo, tatizo ni kwamba tunajiamini kuwa tuko perfect katika kila jambo tunasahahu ya kuwa sisi ni mwili wa kristo .. Kila mmoja anaweka jitihada ya kufanya vema sio kama wajibu ila ni ili aonekane kuwa bora kuliko fulani, tunasahau kuwa biblia inasema tuwahesabu wengine kuwa ni borá kuliko sisi. siô kwamba tunashindwa kujenga Gorofa uwezo tunao ila tatizo ni Kwamba kila mtu anataka ajenge msingi.. Siô kila kiungo Katika mwili chaweza kuonekana viungo vinginé katika mwili havionekani na kutokuonekana kwake hakumaanishi kuwa viungo hivyo havina umuhimu, wakati mwingine vyaweza kuwa nã umuhimu kuliko hata vinavyoonekana ...
Yamkini wewe ni moyo, au ni kwapa 😂😂😂 . Hapo ndipo umeitiwa sasa usijilazimishe kuwa jicho uonekane maana yeye aliyekuweka hapo kakuweka kwa kusudi..
Kila mtu kuna huduma Mungu kamuitia kwayo,
Inaweza kuwa inafahamika kwa watu wengi au haifahamiki, lakini kufahamika au kutokufahamika hakudetermine ukubwa wa huduma..
Yamkini watu hawakujui lakini kuna kazi kubwa sana unaifanya katika kuujenga ufalme wa Mungu. Nã kupitia hiyo Mungu anajivunia..
Lengo langu katika ujumbe huu ni hili..
Kila mtu amuhesabu mwenzake kuwa ni borá kuliko yeye.. Nã tusifanye huduma kwa mashindano kwa nia ya kuonekana kuwa borá kuliko fulani.. Ila tufanye kama viungo katika mwili wa kristo.. Mwingine anapoinuliwa basi kusiwe nã wivu ila furaha nã shukrani kwasababu aliyeinuliwa ni kiungo ndani ya mwili wa kristo.. Mwingine anapoanguka isiwe chanzo cha kuthibitika kwa unabii ila kila mmoja asikie kuugua juu ya anguko la kiungo ndani ya kristo.. Kama vile ilivyo katika mwili kidole kikiumia mwili wote huuma .
Tusipopendana sisi kwa sisi hatuwezi kumpenda Mungu.. Sababu Mungu ni Pendo..
Tupendane tuchukuliane, tusameheane.. Hakika tutafika..
Kila mtu amkubali tu mwenzake katika eneo au karama Mungu aliyompa.. Kama wewe ni muhubiri basi fanya iliyo nafasi yako.. Kama wewe ni pianist vivyo hivyo.. Sasa sio unakuta pastor ndo muimba kwaya.. Ndo muhazini wa kanisa, ndo pianist wa kanisa, ndo mshauri, mwalimu.. Muinjilisti etc nooo.. Hatuwezi kuwa perfect katika kila eneo.. Maeneo Mengine tuwaachie wale wenye wito huo wakafanya😍😍
Ubarikiwe
Waweza like page yangu Judith Mbilinyi kwa kujifunza zaidi au
0762372408
judithmbilinyi@gmail.com
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon