Uaminifu

Na Judith Mbilinyi 

Praise the living God🙌🙌🙌
 Kuna kitu nataman kushare pamoja  hapa.. Nimesikia mzigo Sana kukisema.. Naamini Kuna mtu Mungu katamani ujumbe huu umfikie

Kuna mambo mengi tunayapanga na Kuna level kubwa Sana tunatamani Mungu atufikishe Lakini tunachokosa kikubwa ni uaminifu
 Kuna level kubwa Mungu anatamani kutufikisha lakini akiangalia ndani yetu haoni uaminifu, Sikia Kuna level ili uzifikie ni lazima Kuna maeneo utapimwa
 Kama ilivyo katika masomo unapotaka kuingia darasa jingine ni lazima ufanye mtihan vivyo hivyo katika maisha ya Kiroho Lazima Mungu apime uaminifu wako ili kuuthibitisha uhusiano wake kati yako na yeye.. Mungu anachotaka ni kwamba imani yako ijengwe kwake na sio kwenye vitu alivyokupa

 Mungu anachotaka imani yako ijengwe kwake na sio kwenye huduma au Karama au kipawa alichonacho
 Yani Mungu anachotaka kukiona ndani yako ni kwa jinsi gani umemuweka yeye kuwa wa kwanza katika mambo yote
 Hata ukienda kumuuliza leo mwakasege au mtumishi yoyote yule ambaye Mungu anamtumi lazima atakwambia Kuna maeneo Mungu alimpitisha
Na lengo LA kumpitisha huko lilikuwa ni kupima uaminifu wake juu ya kristo
Kama hautakuwa mwaminifu kwa Mungu Kuna mambo katika maisha yako yatabaki kama ahadi
Ibrahim aliahidiwa kuwa Baba wa mataifa lakini bado mke wake alikuwa tasa..
 Ahadi ya Mungu kumbariki Ibrahim kuwa Baba wa mataifa ilikuwa pale pale ijapo mke wake alikuwa tasa
 Kilichofanya Ile ahadi ya kuwa Ibrahim Baba wa mataifa ni pale alipoambiwa amtoe mwana wake kama sadaka
Hapo ndipo ahadi ya Mungu ya Ibrahim kuwa Baba wa mataifa ilitimia
Na inawezekena kama Ibrahim angekataa kumtoa isaka yamkini kuwa Baba wa mataifa ingebaki kama ahadi
 Kuna level fulani za kiroho ili uzifikie ni lazima uchujwe
Na hapo kwenye kuchujwa watu wengi wamebaki nyuma
Ayubu katika utumishi wake wote lakini bado alijaribiwa
 Mungu aliruhusu shetani amjaribu ayubu
 Kilichokuwa kinapimwa pale ni uaminifu
 Ni kwa jinsi gani Imani ya Ayubu imejengwa kwenye Msingi wa Mungu mwenyewe na sio kwenye afya na vitu vionekenavyo
Kumbu Kumbu 13:1-3 Inaelezea Sana hasa ule mstari wa tatu: Kwamba Kuna mambo yaweza tokea kwetu kama majaribu lakini ndicho kipimo Mungu anachotupimia imani Yetu
Ni kweli katika Yakobo biblia inasema Mungu hamjaribu mtu Ila mtu hujaribiwa kwa tamaa yake
Lakini kupitia hayo majaribu ndipo Mungu anapima uaminifu wetu kwake
 Ikiwa tunampenda kwa mioyo yetu yote au hapana Tamaa inaweza kukusababisha ukapoteza vitu vya msingi Sana katika maisha na huduma yako
Kumbuka kwa Esau na Yakobo kilichofanya wauziane uzaliwa kulikuwa ni chakula
 Chakula tu lakini kilipoteza kitu kikubwa sana
: Kumbuka kilichofanya Eve na Adam watolewe edeni (presence of God)  lilikuwa ni tunda  Tu
: Kuna vitu vidogo tunafanya lakini vinatupelekea kupoteza vitu vikubwa Sana vya thamani
 *Na kupitia hivyo vitu ndipo Mungu anapima uaminifu wetu Na kama hatauona uaminifu kwetu basi hatuwezi kupiga hatua katika hayo mambo*
 Suala LA kuwa Mungu amekupangia kuwa na huduma kubwa lipo kama ahadi lakini ili litimie ni lazima upimwe na ukishapimwa inampa Mungu uhalali wa kukupitisha kwenda level nyingine...
: Ukisoma katika Daniel 9:1-2 utaona jinsi utumwa ukivyimopitili kiwango cha miaka ambacho waliandikiwa kukaa utumwani kwa kinywa cha nabii Yeremia
Katika ulimwengu wa Roho Muda wao wakukaa utumwani ulikuwa umeisha lakini bado walikuwa katika Hali ya utumwa.. Daniel anapokuja kusoma vitabu ndipo anajua ya kuwa wamepitiliza miaka ya kukaa utumwani
 Vivyo hivyo inawezekena katika ulimwengu wa Roho tayari Mungu alishakuumbia kuwa na huduma kubwa au kufika level fulani lakini kwasababu vigezo vya kupokea hivyo vitu havipo ndani yako basi inabaki kuwa kama ahadi
 Huwa najiuliza kipind Yesu anazaliwa walikuwepo wanawake wa ngapi?  Na ni kwanini mariam pekee yake ndiye aliyetumiwa kumzaa Yesu?
Mariam alikuwa bikra.. Maana yake Kuna sifa ya kipekee iliyomfanya Mungu kumtumia mariam kumzaa Yesu
 Kuna mambo mengi Mungu amekuwekea katika ulimwengu wa Roho lakini hayo mambo ili yatimie lazima uyawekee mazingira ya kuyapokea
 Usipoyawekea mazingira inabaki kuwa ahadi tu..  Kama ilivyo kuwa kwa Ibrahim mpaka pale Mungu alipompima uaminifu wake katika kumtoa Isaka
 Mungu awabariki Sana..

  Nawatakia wakati mwema..

Facebook | | Instagram || YouTube
Email: judithmbilinyi@gmail.com
Tel: +255 762 372 408

Toa maoni yako hapa

Previous
Next Post »

1 comments:

Write comments