Tukikiri kwamba tu wafuasi wa Kristo, basi tusitende dhambi

Na Doris Makwaya Moses
Kwa sababu TUNAKIRI kuwa sisi ni wafuasi wa KRISTO, basi sisi ni nuru na hatutakiwi kwenda gizani (Yoh 8:12) yaani HATUTAKIWI kutenda dhambi. Dhambi ni pamoja na _Ufitinishaji, Uzinzi & Uasherati, Kiburi yaani kutokutii MAMLAKA zilizowekwa, Uongo, Usengenyaji, Ulevi n.k_*

*TWAWEZAJE KUEPUKA YOTE HAYO???😟😟😟 Hakika peke yetu hatuwezi, tunamuhitaji MUNGU.*
*_Twende kwa YESU tukanywe maji (Yoh 7:37)._ Maji hayo huondoa KIU. Si kiu hii ya maji ya kidunia la! Ni kiu ya DHAMBI. _Tukinywa maji hayo yatafanyika chemchem za UZIMA ndani yetu (Yoh 7:38)._ KIVIPI? Kwa sababu DHAMBI haitotimizwa na SIKU ZOTE, dhambi MATOKEO yake ni mauti. Au tumesahau kuwa mshahara wa DHAMBI ni mauti (Rumi 6:23)???*

*_Lakini zaidi sana YESU alituahidia msaidizi ambaye huyo hutuongoza ktk kweli yote._ Yeye hutupa NGUVU ya kushinda yale yaonekanayo kutokuwezekana. Mpenzi nakusihi, ukae na unyenyekee kwa Yesu hata ujazwe huyo ili upokee nguvu. (Mdo 1:8)*

*Mungu atubariki, Mungu atutunze na Mungu atuongoze, amen*
Previous
Next Post »