Kutengwa kwa Walawi 1

Na Norangel Benard.
Neno la ufunguzi, utangulizi

Hesabu 8:5-18 

“5Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 6Watwae Walawi na kuwaondoa kati ya wana wa Israeli, kisha uwatakase.7Nawe utawafanyia mambo haya ili kuwatakasa; nyunyiza juu yao maji yatakasayo dhambi, nao wajinyoe kwa wembe mwili wote, kisha wazifue nguo zao, na kujitakasa. 8Kisha na watwae ng’ombe mume mmoja mchanga, na sadaka yake ya unga, unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, nawe utatwaa ng’ombe mume mchanga mwingine kuwa sadaka ya dhambi. 9Nawe utawahudhurisha Walawi mbele ya hema ya kukutania; nawe utaukutanisha mkutano wote wa wana wa Israeli; 10nawe utawahudhurisha Walawi mbele za BWANA; kisha wana wa Israeli wataweka mikono yao juu ya Walawi; 11naye Haruni atawasongeza Walawi mbele za BWANA wawe sadaka ya kutikiswa, kwa ajili ya wana wa Israeli, ili wawe wenye kufanya utumishi wa BWANA. 12Kisha Walawi wataweka mikono yao juu ya vichwa vya hao ng’ombe; nawe umtoe mmoja kuwa sadaka ya dhambi kwa BWANA, na huyo wa pili awe sadaka ya kuteketezwa, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya Walawi. 13Kisha utawaweka Walawi mbele ya Haruni, na mbele ya wanawe na kuwasongeza kwa BWANA wawe sadaka ya kutikiswa.14Ndivyo utakavyowatenga Walawi na kuwatoa katika wana wa Israeli; na Walawi watakuwa wangu. 15Kisha baadaye Walawi wataingia ndani, ili wafanye utumishi wa hema ya kukutania; nawe utawatakasa, na kuwasongeza wawe sadaka ya kutikiswa. 16Kwa kuwa nimepewa kabisa mimi watu hawa kutoka katika wana wa Israeli; badala ya wote wafunguao mimba, maana, wazaliwa wa kwanza wa wana wa Israeli wote, nimewatwaa wawe wangu. 17Kwa kuwa wazaliwa wa kwanza wote katika wana wa Israeli ni wangu, wa wanadamu na wa wanyama; siku hiyo niliyowapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri niliwatakasa kwa ajili yangu mwenyewe. 18Nami nimewatwaa Walawi badala ya wazaliwa wa kwanza wote walio katika wana wa Israeli.”

Image result for levites in the bible
Nataka tujifunze kutoka kwa Walawi, naamini wote tumeshasikia habari za walawi. Hawa Mungu aliwatenga maalumu kwaa ajili ya kazi yake maalumu, sisi kama walawi wa kipindi hiki nini tunapaswa kujifunza kutoka kwa hawa?
Mungu ametupa UPENDELEO MKUBWA SANA wa kumtumikia yeye katika madhabahu yake, ametuheshimu na kutuheshimisha. Siyo kila mtu alifanya kazi walizozifanya walawi ila walawi pekee.
Walawi wakiwekwa katika nafasi ya kwanza pamoja na makuhani, na walikuwa wakifanya kazi na kutumika pamoja na makuhani. Walikubali kuwa chini ya kuhani ambaye ni Haruni aliyekuwa napewa maelekezo na Musa kutoka kwa Mungu.

Je Walawi walitoka wapi?
Previous
Next Post »