Kutengwa kwa Walawi 2

Na Norangel Benard
Walawi walianzia wapi?
Mwanzo 29:34

Akapata mimba tena, akazaa mwana, akasema, Basi wakati huu mume wangu ataungana nami, kwa sababu nimemzalia wana watatu. Kwa hiyo akamwita jina lake Lawi.
Tunaona hapa Habari za Yakobo na wake zake, Lea na Rahel, Yakobo alifanya kazi kwa labani kwa lengo la kumpata Rahel lakini akapewa Lea, na baadae akaongeza muda wa kutumika akampata aliyemtaka Raheli. Tunaona mstari wa 31; Kabisa Yakobo hakuwa amempenda Lea na Bwana alilijua hilo, akaamua kufunga tumbo la Rahel, Mungu akaamua kumbariki Leah akapata watoto, ukiangalia majina ya watoto wa Leah yamebeba maana soma mstari wa 31-34, alikuwa anawapa watoto wake majina kwa kumtukuza Bwana.
 Reuben- kwa kuwa BWANA AMEONA teso langu
 Simeoni- kwa kuwa BWANA AMESIKIA ya kwamba mimi sikupendwa, amenipa na huyu  Lawi- basi wakati huu mume wangu ATAUNGANA nami,
  Yuda- akasema mara hii NITAMSIFU BWANA

Tunajifunza nini kwa Lea?
Leah alikuwa akiishii ibada, kwa kile ambacho Bwana alifanya alimtukuza na kumtukuza. Mungu anapendezwa na sifa na anaketi juu ya sifa za watoto wake. Mungu aliendelea kumbariki Leah kwasababu Leah aliijua siri iliyoko ndani ya kumsifu Bwana (IBADA). Hapo ndipo tunaona jina LAWI linaanza.
LAWI maana yake nini?
Angalia mstari wa 34,
KIUNGANISHI, SABABISHO LA MUUNGANIKO
Kuzaliwa kwa Lawi kulileta furaha ndani yao kwa kuwa Leah aliona sasa ataungana na mumewe kwasababu amemzalia mtoto wa tatu. Huyu Lawi alianza kuwa baraka tangu azaliwe, mama yake alimtamkia baraka kuwa yeye atakuwa sababu ya kuunganisha vilivyotenganishwa.. (Nguvu katika maneno tuyatamkayo). Ukitamka mema na baraka zitakuja, lakini ukitamka mabaya na laana zitakuja. Tujifunze kutamkia watoto wetu baraka na yaliyo mema. Sasa hapo ndipo tunaona LAWI na kabila la WALAWI lilipo anzia.
                            Image result for levites in the bible
Mungu ananena na Musa anamuagiza kuwa walawi watengwe.

1. WALAWI TUMETENGWA NA KUTAKASWA KWAAJILI YA BWANA
Haruni anaambiwa awatenge kabila la walawi, awatakase, wafue nguo zao, na wanyolewe mwili mzima.

Kwanini?
Hii ni ishara ya utakaso, ukivitenga vyombo vya thamani utahakikisha umevisafisha vizuri, utavisafisha kwa umakini sana kwamaana ni vyombo vya thamani, utavikagua uone hata kama kuna ka punje ka uchafu, hivi ndivyo Mungu alivyowatazama walawi na hivi ndivyo anavyotutazama walawi wa kizazi hiki.
Tutambue kuwa tumetengwa, hatupaswi kuchangamana na uchafu tena, sisi ni vyombo vya thamani, tukubali kukaa pale ambapo Mungu anataka tukae alipotuweka, kama atatuweka kwenye kabati lake la thamani tukae humo, usijichanganye na kurudi kukaa kwenye beseni la vyombo.
Kilichotengwa ni cha thamani, hatupaswi kuwa na uchafu wa aina yoyote, kunyoa nywele mwili wote ni kujikagua kabisa na kuhakikisha uko safi kila eneo katika maisha yako kiroho, kimwili na kimawazo/akili.
Kufua nguo ni kutoa uchafu wa mabaki ya maisha yako ya dhambi ya nyuma na kuanza upya na Yesu.
Hatutupi nguo zikichafuka ila tunazifua zikatakata na tunavaa tena, yawezekana umeishi maisha machafu sana nyuma lakini baada ya kujitambua kuwa umetengwa na kutakaswa kuwa chombo cha heshima unaanza kuishi maisha mapya.
Kuendelea kunyoa mwili wote kila siku, ni kujihakiki kila siku maana nywele tunanyoa halafu huota sasa ni kuwa makini kujilinda nafsi na mioyo yetu kuangalia ni wapi nywele zimeanza kuota na kuzinyoa mara moja.
Mlawi hapaswi kuichekea dhambi, unapogundua umekosea tengeneza haraka sana, usijifiche maana Bwana amekuweka mahali pa kuonekana uchafu utaonekana na utajiaibisha na kumuaibisha aliyekuweka mahali pa heshima.
JITAMBUE Mstari wa 5-8👆�👆�
Kama wote tutakuwa tunapitia biblia itanipa urahisi wa kuelezea pasipo kufanya marejeo “reference”.  

2. WALAWI TUKO KUMTUMIKIA MUNGU KWA KUWATUMIKIA WATU ALIYOTUPA MUNGU TUTUMIKE KWAO
Mstari wa 9-11
Mungu anamuagiza Musa awalete WALAWI mbele ya hema ya kukutania (huduma ya kuonekana) na utawakutanisha na wana waisrael wote, halafu awahudhurishe walawi mbele za Bwana wakati mkutano wa wa wana wa Israeli uko hapo na walawi wapo hapo, halafu anaagiza wana waisrael watawawekea mikono walawi.  
Kwanini kuwekwa mbele za wana wa Israel? Kwanini kuwekewa mikono?
Baraka za Walawi ziko katika nyumba ya Israel, Walawi waliingia katika hema ya kukutania kama wawakilishi wa wana wa Isreal pamoja na Kuhani Haruni, walikuwa wanamtumikia Mungu kwa kuwatumikia watu wa Mungu. Kwahiyo Baraka za Walawi zilikuwa zimefungwa katika mikono ya wana wa Israeli, kwamaana kama wana wa Israel wasingekuwepo basi walawi wasingehitajika.
Imetupasa kuwaheshimu na kutumika kwa UNYENYEKEVU mkubwa, na kuishi na watu kwa akili na lazima maisha yetu yawe kielelezo bora, asiwepo atakaeonekana kuwa kwazo au ubaya, pia tufahamu hii ni huduma ya kuonekana, kuwa makini sana kwa namna unavyojiweka kwa watu, hata physical body language yako isome vema, usiigize lakini hayo yawe maisha yako, kuwa makini kile kilichomo ndani yako ndicho tukione na nje.
3. MLAWI NI MALI YA MUNGU MWENYEWE
Mstari wa 13-18
MUNGU anaonyesha msisitizo kuwa walawi ni wake,  
Eh Mlawi, tambua kuwa maisha yako si mali yako, "Your life is not your Own". Hauna sauti yoyote juu ya maisha yako zaidi ya yule aliyekuumba na kutangaza kuwa anakumiliki na wewe ni wake. Hivyo basi;
 UTAISHI KAMA MUNGU ATAKAVYO.
  UTAENENDA KAMA MUNGU ATAKAVYO.
 UTAMTII MUNGU KWA KILA JAMBO.


Sisi waimbaji tunakasumba moja yani kila tukio “event” lazima tuwepo, kila nyimbo lazima nishirikishwe, kila madhabahu ya kila kanisa lazima nisimame, nani amekuruhusu wewe? Kwanini unajiamulia utadhani ulijichagua mwenywe,
KILA ANAYEABUDU “WORSHIPPER” AJENGE TABIA YA KAMUULIZA MUNGU
Je, hiki nifanye au nisifanye? Hapa niende au nisiende? Je, huu ni wakati wa kufanya tamasha au sio? Je, huu ni wakati wa kutoa albamu au je, leo niimbeje? je, leo nileje au leo nivaaje?
JENGA NA KUIMARISHA USHIRIKA WAKO NA ROHO WA MUNGU
Usiishi ishi tu, wewe ni wathamani, sio lazima kila sehemu uwepo, sisemi usishirikiane na watu au usichangamane na watu hapana, lakini pata ruhusa kwa ya aliyekutenga na kukupa hiyo neema usiishi kiholela.
SAUTI SIO YAKO, MWILI SIO WAKO, KILA ULICHONACHO NI CHA BWANA, NI CHAKE.

Pakua Mafundisho yote hapa 
Previous
Next Post »