Ufute Alama_Edward Kisusu ft. Christopher Mwahangila

Huu ni wimbo unaotambulisha Albamu mpya ya mwimbaji chipukizi Edward Kisusu akimshirikisha Christopher  Mwahangila.
Akiongea na Sound Of Worship kuhusu kumshirikisha Christopher Mwahangila katika Album yake mpya, Edward Kisusu amesema
  "Kaka Christopher ni rafiki yangu ninayempenda sana na pia ni kaka yangu ambaye nimefanya naye huduma sehemu mbalimbali kwa muda mrefu. Nimemjua toka zamani sana kama mtumishi mnyenyekevu na jinsi anavyompenda Mungu." 
 Edward Kisusu anatambulisha wimbo huu ambao tayari uko katika mfumo wa audio. Anatarajia kutoa video ya wimbo huu mapema.
  Huu hapa chini ni wimbo wake unaobeba albamu yake mpya "UFUTE ALAMA", sikiliza, pakua na mwachie maoni yako, washirikishe na wenzako.
 Album hii pia ina nyimbo nyingine nyingi na moja ambayo mwenyewe anasema anaipenda ni hii ya "Atanijibu" . Akizungumzia Album yake iliyopita mwimbaji huyo hakusita kuzungumzia jinsi wimbo wake uliobeba Album yake "Ni wewe umeniita" ulivyopendwa sana na mashabiki wake na wapenzi wa mziki wa injili Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Download


Facebook | Twitter | Instagram | YouTube
Email: edwardkisusu@yahoo.com
Tel: +255 764 899 489

Mwachie maoni yako hapa


Previous
Next Post »