MSAMAHA WA KWELI

Kuna hekima ambayo imekuwa ikitumika, nayo yasema ukitaka kutofautisha halisi na isiyo halisi basi ijue halisi vizuri. Basi ngoja leo nijifunze halisi (original) ya Msamaha. 

Msamaha halisi na wa kweli ni ule:
1. Wa gharama: Ilimgharimu Yesu kuacha utukufu, enzi na utajiri juu mbinguni ili mwanadamu asamehewe. Ilimgharimu Yesu maisha yake ili kulipa gharama ya msamaha wa mwanadamu. Unapotaka kusamehe usianze kuhesabu gharama, kwa kuwa hata sasa Msamaha wa kweli ni Gharama. 

2. Hutolewa bure kwa yule anayeupokea: Ilimgharimu Yesu maisha yake ili kumsamehe mwanadamu lakini haikumgharimu mwanadamu chochote kuupokea msamaha huo. Yesu aliutoa msamaha kwa mwanadamu bure. Hakuhitaji mwanadamu alipe chochote ili aupate msamaha alioulipia gharama kubwa. Unataka kusamehe fahamu hili, husamehi ili ulipwe ama upokee kitu. Msamaha wa kweli hutolewa bure kwa yule anayesamehewa. 

Tukutane Alhamisi ijayo..

 #SAMEHE, ISHI SALAMA
Goodluck Ernest, 2016
+255 713 660921
mashambo.ge@gmail.com
Previous
Next Post »