Maisha ni fumbo

Na Gladness Munisi

Kuna watu leo unaweza ukawatafuta kwa bidii wakawa wanakukwepa na kukudharau kwa kuona hauna future.Ila kuna siku watakutafuta uwasaidie.

Maisha ni Fumbo,Jifunze kuheshimu kila mtu hata kama unaona hana kitu.

Nawe usijisikie vibaya unaponyimwa nafasi unayotaka.Wakati mwingine Mungu huwa anataka kuwafundisha kitu watu wenye kiburi ambao hudhani wengine hawana nafasi ya kufikia kuwa kama wao.Anachofanya ni kuwatendea wale wanaodharauliwa kufikia juu zaidi kuliko wale wanaowadharau.

Uzuri ni kuwa,kusudi la Mungu juu ya maisha yako haliwezi kuzuiwa kwa mtu kukataa kuwa Msaada kwako.Ukiona mmoja amekataa ujue Kuna Mwingine Mungu amemwandaa kwa ajili yako-Ukikata tamaa hata huyo mwingine aliyeandaliwa hautamuona ila ukiendelea kutumaini Mungu atamleta kwa majira yake.

Shikilia Ndoto Yako,Hatima Yako ni Kubwa Sana.

See You At The Top

#DontSlowDown
#NeverGiveUp
#ItsNotOvetYet


#TIMIZAMALENGOYAKO
Previous
Next Post »