SIRI YA MAISHA

Na Judith Mbilinyi 

leo nianze kwa kuuliza maswali machache tu.. Je nini kitafutata kwako baada ya maisha yako ya hapa duniani??
Je Jina lako linafahamika mbinguni  kama unavyofahamika duniani??
Utajisikiaje pale ambapo utakuwa na jina kubwa duniani lakini mbinguni hufahamiki??
Kufanya mambo makubwa na ya ajabu sio ishara tosha ya kukuthibitisha kuwa unatambulika mbinguni...
Kunawakati unaweza kutumika kulipitisha kusudi la ki Mungu lakini mbinguni kukawa hakuna document ya jina lako... ✏
Ngoja nielezee kwa mfumo mwingine tena.. Rahabu alikuwa kahaba lakini ukahaba wake haukumzuia kutumika kuwatunza wale watu walioenda kuipeleleza nchi ya ahadi..
Yuda alikuwa mwanafunzi wa Yesu lakini alikua msaliti na usaliti wake ulifanya Yesu kusulubiwa kwaajili ya makosa yetu...
Kutumiwa kupitisha kusudi la kiMungu kwa kutumia ubora au udhaifu ulionao sio ishara tosha kukuthibitishia kuwa jina lako limeandikwa mbinguni
 Luka 10:19 "Tazama nimewapa amri ya kukanyaga nge na nguvu zote za yule adui wala hakuna kitakachowadhuru.. 20 lakini msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii bali furahini kwasababu majina Yenu yameandikwa mbinguni"
.
Kufanya ishara.. Au kuponya watu sio ishara ya kukuthibitishia kuwa Jina lako limeandikwa mbinguni..
Pasipo utakatifu hakuna atakayemuona Mungu... Kuwahubiria wengine au kuimba au kutoa sana sadaka au kufanya mambo makubwa,  miujiza n. K sio tiketi ya kuingia mbinguni ila kinachoangaliwa hapa ni utakatifu.. Kama hakuna utakatifu hakuna kumuona Mungu... Na ndo maana Yesu alisema kuwa wengi watakuja siku ile wakisema Bwana kwa Jina lako tulitoa pepo lakini atawaambia ondokeni kwangu siwajui ninyi....

Maisha yamebeba siri kubwa sana... Maisha sio kama line ambayo ukiipoteza unaweza kurenew.. Maisha sio kama mitihani ya kidunia ambayo ukifel unaweza ku reset au kufanya supplimentary au ku carry,  maisha  ni kama kalamu isiyo na ufutio.. Ikiandika imeandika..
Ufutio wake ni Damu ya Yesu pekee..
 Kuishi kwako duniani kumebeba kusudi la kiuungu Je ni kwa jinsi gani unatumia neema ya uhai katika kulitimiza kusudi la Mungu hapa duniani.??
 HIVI UNAJUA KUWA KUNA WATU WANATAMANI WANGEPEWA HATA DAKIKA MOJA WARUDI DUNIANI KUTENGENEZA MAISHA YAO??  KWANINI TUNACHEZEA NEEMA YA WOKOVU NA UHAI TULIONAO...?
KWANINI  HATUITII SAUTI YA MUNGU?
KWANINI TUNAJITAHIDI SANA KUWAPENDEZESHA WANADAMU KWA JITIHADA ZOTE TUNASAHAU KUMPENDEZA MUNGU??

Yesu anasema kama mwenye nyumba angalitambua saa ya mwivi ajapo angalikesha usiku kucha... Yesu atakaporudi duniani hatorudi kwa hali ya umasikini kama dhaman ila kwa kuzionesha nguvu zake duniani.. Kipindi tulichonacho ni kipindi cha neema na kuna wakati kipindi hiki cha neema kitapita... Ambako utatamani kuokoa haitawezekana..

Swali la kujiuliza hivi baada ya maisha ya hapa duniani utakuwa mgeni wa nani?
Kuzimu au  mbinguni?  Je wale uliowahubiria watajisikiaje watakapoona kuwa nawewe ni mmoja wa walioachwa!??
Tunatumia muda mwingi kuwaimbia wengine.. Kuwahubiria wengine,  kuwafundisha wengine
 Kwa habari za kristo lakini je ni kwajinsi gani tumeendelea kuutunza utakatifu ambao pasipo huo hakuna atajayemuona Mungu??
Sikia Mungu hatokuuliza uliwahubiria watu wangapi au ulitoa albamu ngapi au una vitabu vingapi ila UTAKATIFU ndiyo tiketi yako ya kuingia mbinguni... Hayo mengine ni kuikuza tu taji utakayopewa

Ufunuo 16:15 "Tazama naja kama mwivi Heri akeshaye na kuyatunza mavazi yake asiende uchi hata watu wakaione aibu yake"

Yesu anarudi na tena ujio wake ni kama Mwivi Je unatamani watu kuiona aibu yako??
Sikia ni kwambie aliposema mmoja atwaliwa mmoja aachwa haikuwa na maana tu unyakuo wa siku ya mwisho ila ni hata katika maisha yako hapa duniani ... Unaweza kujiuliza ni wangapi umesoma nao au umeishi nao hawako tena duniani??  Wengine walikua ni marafiki zako lakini wamesha twaliwa .,  wewe ni mmoja kati ya waliopata neema ya kuwa hai duniani  swali la kuiuliza je unaitumiaje neema ya uhai uliyopewa na Mungu katika kuutunza utakatifu??

CHAGUENI HIVI LEO NINANI MTAKAYEMTUMIKIA..
Mungu hapendi mtu mwenye michanganyo... Ukiwa vuguvugu atakutapika... Ni vema tu ikiwa umechagua kumtumikia Kristo basi mtumikie kwa jitihada zote huku ukijua ipo thawabu mbinguni...

Ufunuo 22:11 "Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu na mwenye uchafu na azidi kufanya uchafu,  mwenye haki na azidi kufanya haki na mtakatifu na azidi kutakaswa"

Ikiwa tumekubali kumtumikia Yesu basi tumtumikie kwa mioyo yetu yote.. Roho. zetu zote... Acha ulimwengu utuone kama wajinga lakini tunamjua Mungu tunayemtumikia na tuna uhakika wa kuyarithi yale makao ambayo Yesu  anatuandalia...
Kumbuka ni bora ulimwengu usikufahamu lakini mbinguni ukafahamika... Ni bora ukashindwa kuwa na jina kubwa duniani lakini Jina lako likawa linafahamika mbinguni...lakini ni Aibu kuwa na Jina kubwa duniani lakini mbinguni ukawa hufaamiki,   Kumbuka maisha ya duniani ni ya muda mfupi lakini yako maisha yadumuyo ... Ni bora ukavumilia dhiki chache utakazopata duniani lakini ukapata maisha ya umilele mazuri yadumuyo "Duniani mnayo dhiki lakini jipeni moyo,  mimi nimeushinda ulimwengu"

Mungu atusaidie kuutunza utakatifu
         AMINA

@Judith_mbilinyi
judithmbilinyi@gmail.com
0762372408

Kama unahitaji kuokoka basi tuwasiliane kwa namba hiyo hapo juu
Previous
Next Post »