EPUKA KULALAMIKA.

Na Judith Mbilinyi

Kulikua na dada mmoja ambaye alitamani sana miaka ya mbeleni aje kufika nje ya nchi (ulaya) hiyo ilikua ni ndoto yake na hamu yake kubwa .. Na hata alipokua akikaa na wenzake alikuwa akiwaeleza juu ya hamu yake kubwa ya kufika ulaya... Miaka ikaenda yule dada akajibangaiza kutafuta hela kwa jitihada zake zote na alifanikiwa kupata pesa ambayo ingeweza kukidhi nauli ya kwenda ulaya na kurudi pamoja na pesa ya mahitaji mengine..
Alifurahi sana kupata pesa na moyoni aliona kuwa ndoto yake ya kufika ulaya imekamilika..
Baada ya siku kadhaa alianza maandalizi kwa ajili ya safari ikiwapo kukata tiketi . VISA  na passport kwaajili ya safari ya kuelekea ulaya..
Ndani ya moyo wake alijawa na furaha sana na kila aliyemuona alimuhadithia juu ya maono yake na kuhusu safari hiyo... Siku ya safari ilifika  akajiandaa kwenda Airport (uwanja wa ndege) akiwa amebeba begi kubwa la nguo na kipochi kidogo mkononi... Wengi huita kipima joto... Alipofika airport alikaguliwa na mizigo mingine ikawekwa eneo husika kwaajili ya safari .. Akiwa pale airport wakati akisubiri muda ufike ili akapande ndege gafla kibaka alitokea na kupora kipochi chake alichokua amekibeba na kuondoka nacho.. Masikini yule dada alilia sana kwasababu kile kipochi kilikua kina tiketi.. Passport na baadhi ya taarifa juu ya safari yake pamoja na pesa za kujikimu... Yule dada alilia sana... Akaenda kwenye kituo cha polisi kilichokuwa hapo airport na alipofika hapo akawaeleza juu ya kuibiwa kwa kipochi chake pamoja na vitu vya msingi vilivyokua ndani ya kile kipochi... Wale askari wakaanza kupeleleza na kumsaka mwizi..
Wakati huo ndege ilikua imebakiza dakika tano ili kuruka.. Yule dada alilia sana.. Aliona kuwa ndoto zake ndo zimeishia pale.. Alimlaani sana yule mwizi kwa kitendo alichomfanyia.. Pia aliwaza itakuwaje rafiki zake wakimuona anarudi .. Wakati anawaza hayo yote muda wa ndege kuondoka ulifika na kwasababu yule dada hakuwa na taarifa za kimsingi zinazomsibitisha  kuwa alikata tiketi ile ndege iliondoka ikamuacha... Yule dada alilia sana.. Alijilaumi sana huku akimlaani sana yule mporaji.. Baada ya dk 15 mwizi alikamatwa akiwa na pochi pamoja na zile taarifa za kimsingi za yule dada.. Pesa na tiketi na passport na wakati wakiendelea kumhoji yule mwizi na kupanga juu ya adhabu watakayompa ghafla taarifa za kusikitisha zilifika pale airport kuwa ile ndege iliyoondoka muda mfupi imepata ajali na abiria wote wamefariki... Yule dada alishanga sana na ghafla alichukua nusu ya pesa iliyokuwa kwenye pochi yake na kumpa yule mwezi kama ishara ya kumshukuru kwa kuyaokoa maisha yake.. Maana kama mwizi asingeiba ile pochi basi yule dada angepanda ile ndege na angeenda kufia kwa ajali...

Hadithi hii inatufundisha nini..
Kuna watu wanaweza kutokea kwetu kama vizuizi vya ndoto zetu kutimia lakini ukweli ni kwamba Mungu huwatumia hao kutuweka salama na kutuepusha na mambo mabaya...
Maadui wengine katika maisha yako wapo kukusaidia kufikia hatua fulani ya kimafanikio.. Epuka kulaumu juu ya ugumu fulani unaopitia.. Huwezi jua ni kwakiasi gani MUNGU anakutetea..
Maadui wanaweza kuona kuwa wanakukomoa kukufanyia ubaya lakini ukweli ni kwamba wanakusaidia kulitimiza kusudi la Mungu...
Ukimpiga chura teke unaweza kuhisi kuwa umemkomoa kumbe unampunguzia safari.. Yani umemrahisihia kufika mapema .. Ndivyo ilivyo kwa maadui .. Wao wanaweza kuhisi kuwa wamekukomoa lakini kumbe ndo wanakusaidi kulifikia kusudi lako...
Jifunze kwa Yusuph... Ndugu zake walipomuuza walihisi wamemkomoa kumbe ndo walikua wanamsogeza kufikia maono yake ya kuwa waziri......

ni kweli kuna wakati unapitia magumu na shida ambazo zinakupelekea kuhisi kuwa labda Mungu amekusahau.. Lakini leo ni kutie moyo ya kuwa katika ugumu wowote unaoupitia bado Mungu anakuwazia mema na bado yupo upande wako...

@Judith_mbilinyi
0762372408
judithmbilinyi@gmail.com

Ninaandaa kitabu chenye kichwa kinachosema #NAMNA_YA_KULITAMBUA_KUSUDI_LA_MUNGU

hii ni baadhi ya part iliyopo kwenye kitabu hicho...
Kama kuna kitu umejifunza basi comment nimejifunza pia share uwezavyo ujumbe huuu

UBARIKIWE
Previous
Next Post »