Peace Donatus

Peace Donatus ni mwimbaji chipukizi wa nyimbo za injili kutoka nchini Tanzania. Alianza uimbaji tangu akiwa mdogo. Akiwa na umri wa miaka tisa (9) tu alifanikiwa kuunda band ya muziki iliyokuwa inaitwa UTULIVU BAND na katika umri huu alianza kutunga na kuimba mwenyewe. Wimbo wake wa kwanza ulikuwa unaitwa NI YESU. Band yake ilivunjika tu mara baada ya wote kwenda masomoni. Akiwa na umri wa miaka kumi na sita (16) alianza tena huduma ya uimbaji.



Peace Donatus alirekodi video ya NIFICHE BWANA mwaka 2014 na baadae aliendelea na masomo yake. Anawashukuru wote ambao wanaendelea kumsaidia kwa ukaribu sana hasa wazazi wake na Buzu Tv Online.
 Peace anamshukuru Mungu kwa kumsaidia kurekodi wimbo mwingine wa video, NAKUPENDA YESU ambao ameuachia mwaka 2018.




Peace Donatus anamshukuru Mungu kwa hatua aliyoifikia. Anatamani kufika mbali sana zaidi katika huduma hii ya uimbaji wa nyimbo za injili. Lengo kubwa ni kufikisha injili kwa watu wengi kwa njia ya uimbaji. Anayoshauku kwamba Mungu amtumie apendavyo kama chombo chake kufikisha injili kwa watu wake.

Anakumbana na changamoto nyingi kama pesa kwaajili ya uendeshaji wa huduma hii ya uimbaji na wasambazaji wa kazi zake kufikia sehemu ambazo Mungu amekusudia zifike. Changamoto hizi anajitahidi kuzikabili kwa kwenda mwenyewe kuitangaza huduma yake, pia anafanya maombi ili Mungu aweze kumfanikisha. Familia yake na wadau mbalimbali wanamchango mkubwa sana katika huduma yake kwa ushauri, mafundisho na mchango.

Hadi sasa anazo nyimbo tisa (9) kwenye mfumo wa audio, na kati ya hizo tayari ameshatengeneza video mbili (2). Hana Albam, lakini anategemea kutoa albam hivi karibuni Mungu akimsaidia.

Mawasiliano:

Instagram | Facebook | YouTube|
Email: peacedon2017@gmail.com
WhatsApp: +255 744 008 503

Previous
Next Post »