Judith Mbilinyi_Mapenzi yatimizwe

    Anaitwa Judith Mbilinyi mwimbaji chipukizi wa nyimbo za injili nchini Tanzania mwenye ndoto za kufika mbali katika fani hii ya muziki wa injili.Ni dada anayependa zaidi kufanya muziki wa "live". Wimbo huu ni moja kati ya nyimbo 11 zinazobeba Albamu yake ya kwanza inayoenda kwa jina la "Wamekosa nini?" ambayo pia iko katika mfumo wa sauti "Audio".  Albamu hii imerekodiwa na Mwebrania Studio iliyoko huko Iringa.
     Akiongea na Sound Of Worship kuhusiana na video ya Albamu hii anasema pesa bado ni changamoto, lakini anatamani zaidi kama angeanza na video za "live". Pia aliongeza kwamba angetamani kutoa Albamu ya pili mapema iwezekanavyo lakini bado changamoto inakuwa bado hawezi kufanya kazi katika ule ubora anaoutaka. Aliongezea kwamba atakuwa anatoa wimbo mmoja mmoja anatulia, na akiamua kufanya albamu, itakuwa ya kurekodiwa moja kwa moja huku akiwa anapiga vyombo vya muziki mbalimbali ikiwa ni pamoja na "guitar" na piano, ambavyo anaendelea kujifunza.

Mwachie maoni yako hapa


Previous
Next Post »