KWA NINI MSAMAHA NI MUHIMU?

Msamaha hukusaidia kukua:
Unaposamehe unapata nafasi ya kuwaza mawazo sahihi na ya uzalishaji tena yenye kukusaidia kukua, tofauti na unapokuwa umebeba kisasi. Msamaha huipa nafasi akili yako kufanya kazi nyingine mbali na kazi ya kuhangaika na maumivu, uchungu na kisasi. Huifanya akili kufanya kazi sawa sawa na inavyotakiwa kufanya. Msamaha huipa nafasi akili ya kuwaza mawazo chanya yatakayokupeka kwenye hatua nyingine tofauti na kutokusamehe ambapo hubeba mawazo hasi tu zaidi sana visasi na uchungu ambavyo kamwe havikusaidii kukua. 

Msamaha huponya:
Kutosamehe kunaenda pamoja na maumivu ya moyo, uchungu, kisasi na mzigo mkubwa moyoni. Hivi vyote huleta matatizo kuanzia ya kisaikolojia hadi matatizo ya mwilini kabisa. Unaposamehe maana yake unakuwa umeng'oa mizizi ya tatizo. Kuna magonjwa mengine hayahitaji kwenda hospitali. Kansa ni ugonjwa mmojawapo unaosababishwa na kutokusamehe. Sasa daktari ni wewe mwenyewe, unataka kupona anza kujipa dozi ya Msamaha. Usipopona rudi muulize Yesu yawezekanaje mambo haya (Mathayo 9:6) 

Msamaha ni kujipa uwezo: 
Unaposamehe unakuwa unajipa uwezo ama nguvu ambazo kabla ulimpa yule ambaye ulikuwa umembeba moyoni mwako. Unaposamehe ghafla unarudisha nguvu ya kuamua nini cha kufanya na maisha yako kutoka kwa yule aliyekukosea. Unakuwa huru na maamuzi sahihi na maisha yako. Unapoendelea kutomsamehe aliyekukosea anakuwa ndani yako na anatawala na kuyamiliki maisha yako kwa maumivu, kisasi na uchungu. Maana yake unakuwa umemkabidhi nguvu zako. Kuzikapata tena basi Samehe. 

Kumbuka: "Msamaha si kusahau. Msamaha ni kuyaruhusu maumivu yakuachie na kuondoka" 

Tukutane Alhamisi ijayo..

#SAMEHE, ISHI SALAMA
Goodluck Ernest, +255 713 660 921 mashambo.ge@gmail.com
Previous
Next Post »