CV NA VIGEZO ALIVYOHITAJI MFALME..
-Wana WA Israel
-Uzao wa Kifalme
-Uzao wa Kiungwana.
-Vijana wasio na mawaa
-Wazuri wa USO
-Wajuzi WA Hekima
-Werevu kwa sababu ya Maarifa yako
-Wenye Kufahamu Elimu...
*Na wote walifundishwa Elimu na Lugha ya Kikaldayo kwa miaka mitatu..
*Posho ya chakula ilitengwa kwa ajili ya Wote.
1⃣ Uwezo unaokuwa nao ndio unakuweka katika nafasi nzuri ya kuipata au kuitumia Fursa inapotokea.. Kama Huna thamani yenye kiwango cha tofauti na wengine kuna uwezekano wa kuikosa FURSA inapotokea.
2⃣ Ni wengi wanaweza kuwa na sifa na vigezo vinavyotakiwa, Lakini UTOFAUTI ulio nao kati ya wengi unakupa nafasi ya kupaa na kuwa Bora kati ya Hao wote.
3⃣ Inawezekana kisiwe kitu kipya, ila kile cha kawaida ukikifanya kwa namna ya tofauti kinakuweka kwenye nafasi ya Kuwa Bora Mara kumi zaidi.
4⃣ Tofauti ilikuwepo kati ya wana WA Yuda, kina Danieli ni MUNGU waliyekuwa naye.
"GOD'S FACTOR"...
A. Hii iliwafanya kufanya mambo ambayo wengine Hawafanyi.
Daniel anaonekana kwa mbele akiwa muombaji, Hii ni tabia ambayo nlikuwa nayo maisha yake yote yangu akiwa kijana.
B. Factor Hii iliwafanya kuwa selective, kwamba ni yapi wafanye na ni yapi wasifanye.
Hii ndiyo iliwafanya wasijinajisi kwa chakula cha mfalme.
C. Walikuwa na UJASIRI wa kuitetea Imani yao na Mungu wao waliyekuwa naye. Yamkini miongoni mwao walikuwemo vijana ambao walikuwa wanamjua Mungu ila Hawakuwa serious.
D. MUNGU aliachilia vitu vya Kimungu ambavyo vina tofauti na vya Dunia hii na Ubora Mara kumi zaidi. Mungu aliwapa uwezo Extra na Hekima itokayo juu..
E. Hii ilifanya Hata Tabia na mienendo yao ya maisha kuwa ya tofauti.
🔑 Zaidi ya vigezo vyote ambayo vinaweza kuitajika popote, Kigezo cha kuwa na Mungu halisi ndani yako ndicho kinaweza kukutofautisha Mara kumi zaidi ya wengine.
🔑 Sio Mungu tu kwa jina, ila Kijana aliyeongeza VIWANGO VYAKE KATIKA MUNGU NA KUTENGENEZA UTOFAUTI KATIKA MISINGI MIZURI YA IMANI KATIKA MUNGU WA KWELI, Lazima awe na tofauti..
📌 Wazuri wako wengi.
📌 Wengi Elimu wako wengi.
📌 Wanaojua kupika wako wengi.
📌 Wife na Husband material wanaweza kuwepo wengi..
📌 Viongozi wako wengi,
📌 Waimbaji wako wengi,
📌 Wapigaji wako wengi,
Na wanaweza kuwa na sifa zinazofanana tu tena nzuri..
Kwenye MUNGU HALISI NA MAISHA YENYE VIWANGO VYA JUU, NDIO WATAKAOKUWA BORA MARA KUMI ZAIDI
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon