Saimon Daud Rweikiza

Saimon Daud Rweikiza ni jina ambalo si geni sana katika muziki wa injili Tanzania. Ni mwimbaji ambaye amejariwa kuwa na vipaji vingi sana. Pamoja na kufanya vizuri kwenye uimbaji pia ni kiongozi wa kikundi cha kusifu na kuabudu “Praise and Worship Leader”, mtunzi na mwandishi wa nyimbo “Song composer and writer”, mtumbuizaji “Dancer”, mshereheshaji “Master of Ceremonies (MC)”, DJ, “A Runner
Amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuchochea karama zake zote na kwasasa tayari ana Albamu moja inayobeba jina “Naitwa mbarikiwa”. Anajulikana kwa jina la uimbaji kama “Papaa Rweikiza”. Amekuwa mwalimu wa kwaya mbalimbali kwa muda mrefu sasa, akiwafundisha nyimbo, uchezaji “steps” na kuwaongoza.
Pia amefanikiwa kuanzisha huduma ijulikanayo kama “The Runner Ministry”



Mawasiliano
+255 653 624 729

+255 768 221 353

Maoni




Previous
Next Post »