Kibali kina nguvu zaidi ya ujuzi

Na Judith Mbilinyi 

Leo nikushirikishe  jambo..  Tambua kuwa kibali kina nguvu zaidi ya ujuzi ulionao,  kuwa na ujuzi pasipo kibali haimfanikishi mtu kufika mbali,  unaweza kuwa na ujuzi (professional)  juu ya Hilo eneo unalolitumikia lakini kama huna kibali bado Jamii haiwezi kukukubali,  mfano mdogo tu .. Hujawahi kusikia watu wanasifa zote za kupata kazi lakini hawapati?  Hujawahi kusikia dada ni mzuri na anasifa zote za kuolewa lakini miaka na miaka inapita haolewi.? Ukikosa kibali maana yake unakuwa unamilikiwa na Roho ya kukataliwa na ndio maana Kuna mambo unaona kuwa ni halali kwako kuyapata lakini huyapati kwasababu tu umekosa  KIBALI,  ninachotamani ujifunze hapa ni kujiombea kibali cha ki Mungu kwa kila unalofanya huku ukitambua kuwa juhudi zako binafsi peke yake haitoshi kukufikisha kule unakotakiwa kufika Ila unamuitaji Yesu akupe kibali kwenye Hilo eneo unalotumika kwalo.
๐Ÿ“Œpasipo kibali unaweza kutumia nguvu nyingi na gharama nyingi sana lakini zisikufikishe kupokea matokeo chanya kwasababu Mungu hajaachilia kibali kwenye Hilo eneo unalotumika kwako..  Tujifunze mifano michache katika biblia..

๐Ÿ“#ESTER
 Ukisoma biblia Inaonesha jinsi mfalme alipokuwa anataka kupata malkia na jinsi mabinti walivyokuwa wakitunzwa ili siku Ile mfalme anapochagua malkia basi waonekane kuwa bora zaidi..  Na Ester alionekana kumvutia sana mfalme.. Na akawa malkia.. Kilichomfanya Ester awe malkia sio kwamba alikuwa mzuri wa sura kuliko wengine, yamkini walikuwepo wazuri zaidi yake.. Lakini kwasababu kibali cha Mungu kilikuwa juu ya Ester ndicho kilichomfanya Ester akakubalika kuwa malkia.. Na Mungu alichokuwa akikiona kwa Ester ni kuwa Ester akiwa malkia atakuja kuwatetea ndugu zake wayahudi ili wasiuwawe..

๐Ÿ“#Daniel_na_wenzake
Ukisoma kitabu cha Daniel utaona jinsi ambavyo mfalme alitoa amri ya vijana wote watunzwe huku wakipewa chakula kizuri na Baada ya majuma kadhaa mfalme atachagua wale vijana wenye sura za mvuto kuliko wengine..  Kina Daniel waligoma kula chakula cha mfalme wakasema kamwe hawatajitia unajisi kwa chakula cha mfalme, na wakamuomba mkuu wa matowashi kuwa wao wale mtama na maji.. Biblia inasema siku Ile mfalme alipokuwa akifanya uchaguzi wa vijana wapi wenye sura nzuri.. Biblia inasema kina Daniel, Abelnego, shedrack walionekana kuwa na Sura nzuri kuliko wengine..
Kilichowafanya waonekane vile kuwa na sura nzuri haikuwa mtama.. Ila ni kibali cha Mungu kilikuwa juu ya Daniel na wenzako..

๐Ÿ“ŒMara nyingi tunatumia jitahidi kubwa sana katika maeneo ambayo Mungu bado hajatoa kibali na ndo maana hatupokei matokeo sawa na tunavyotarajia..  Kibali kina nguvu kuliko ujuzi ulionao.. Kibali kina nguvu kuliko UZURI wa sura ulionao.. Kuna mazingira utapita ambayo kwa sifa za kibanadamu usingeweza kupita yote hayo ni kwasababu Mungu ameachilia kibali..  Kibali ni jambo La msingi sana katika huduma Mungu aliyokupa.. Utaalamu ni mzuri sana lakini Utaalamu pasipo kibali cha Mungu ni bure. Utatumia jitahidi kubwa sana lakini bado haitazailisha matokeo unayoyataka..  Leo Muombe Mungu akupe kibali katika kila eneo unalotumika.. Kama ni muimbaji,  mwalimu, doctor.. Muhubiri  etc...
Mungu akubariki

judithmbilinyi@gmail.com
0762372408
Facebook:Judith mbilinyi
Instagram :judith_mbilinyi
Previous
Next Post »