Kuhusu Judith Mbilinyi

Judith Mbilinyi ni mwimbaji chipukizi wa muziki wa injili nchini Tanzania anayefanya vizuri Zaidi katika fani hii ya muziki wa injili. Amekuwa mwimbaji anayependwa sana na watu kulingana na unyenyekevu wake na kumaanisha kile anachokiimba. Alianza uimbaji akiwa mdogo na akiwa shule ya sekondari Nganza aliweza kuimba na wenzake. Moja ya nyimbo zilizofanya vizuri ni "Shetani tumekupiga kibuti".

Mwaka 2013 Judith Mbilinyi alifanikiwa kurekodi Albamu yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la "Wamekosa nini?" iliyofanywa na Mwebrania Studio ya mjini Iringa. Pamoja na changamoto ya kukosa wasabazaji wa kazi yake, alijitahidi kusambaza mwenyewe kazi yake na kuuza nakala zaidi ya 200.

Akiwa Arusha kimasomo, aliendelea na uimbaji katika vikundi mbalimbali vya kusifu na kuabudu, pia alipata mialiko katika baadhi ya huduma mbalimbali. Baada ya kuhamia Moshi kilimanjaro kimasomo pia, Judith Mbilinyi ameweza kutengeneza wimbo mmoja kinyume na malengo yake ya kufanya albamu ya pili "Live" baada ya kukutana na Producer Erasto aliyemshawishi kufanya wimbo wa "Wewe Uko Hapa" Wimbo huu umefanya vizuri sana kwenye mitandao mingi ya kijamii, ukiwemo mtandao wa kutangaza kazi za wasanii wa muziki wa injili Tanzania na Afrika Mashariki "Gospel Media". Huenda wimbo huo ukaingia kwenye "Gospel Media Awards".


Mawasiliano:
Facebook | | Instagram | YouTube
Email: judithmbilinyi@gmail.com
Tel: +255 762 372 408,+255 712 657 950

Previous
Next Post »