UMEUMBWA KWA KUSUDI

  Na Judith Mbilinyi

SEHEMU YA 1

Kusudi ni lengo, kutengwa wakfu kwa ajili ya kazi fulani, kusudi ni moja ya vitu vilivyo katika ulimwengu  wa Roho, kusudi ni mawazo fulani  ambayo yanaweza kuwa bado hayajadhihirika katika ulimwengu wa Mwili.
    Kila mwanadamu chini ya jua ameumbwa kwa kusudi maalum, hakuna mwanadamu aliyezaliwa bila kusudi, kila mwanadamu kuna lengo ambalo Mungu  alilipanga Ili huyo mwanadamu aje kuliishia hapa duniani,  kwahiyo nikuthibitishie tu yakuwa hujaumbwa kwa bahati mbaya, umeumbwa  kwa kusudi,  haijalishi ulizaliwa katika mazingira ya namna gani,  labda Mamá yako alibakwa nã  ndipo ukazaliwa wewe  au mama yako alipata ujauzito bila kukusudia yote hayo hayawezi kuzuia kusudi la Mungu,umeumbwa kwa Kusudi, haupo  duniani kwa bahati mbaya, lipo kusudi  la kiungu juu ya kuumbwa Kwako.

    UUMBAJI WA MWANADAMU

Ukisoma kitabu cha mwanzo 1:1-25
Utaona jinsi Mungu alivyokuwa akiumba vitu mbalimbali, Alikuwa anasema naiwe, kisha inakuwa, lakini katika mwanzo 1:26-27

"Mungu akasema , nã tumfanye mtu kwa mfano wetu,kwa sura yetu, wakatawale samaki wa baharini nã ndege wa Angani, nã wanyama,  nã nchi yote pia, nã kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi, Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimuumba mwanamume nã mwanamke aliwaumba "

Ukisoma katika mwanzo 1:1-25
Mungu alikuwa anasema naiwe Angá inakuwa, bahari n. k inakuwa lakini ilipofika kwa mwanadamu bíblia inasema  "Mungu akaumba mtu kwa mfano wake " Hapa Mungu hakusema nã awe mwanadamu Ila Bíblia inasema AKAUMBA,  hii inaonesha ni jinsi Gani Mungu alivyomthamini mwanadamu,,  alivyomuheshimu
   🔨Mungu hakumumba mwanadamu Kwanza ila alianza kumuumba mtu, yani Mungu  alimuumba mtu katika ulimwengu wa Roho  kabla mwanadamu hajatokea katika ulimwengu wa mwili.. Kwa namna nyingine mwanadamu ni udhihirisho wa mtu akiyeumbwa katika ulimwengu wa Roho kwanza,
Kunatofauti kati ya mtu  nã mwanadamu
Mtu ni muunganiko wa Roho +Nafsi
Mwanadamu ni muunganiko wa Roho+nafsi+mwili
Kwahiyo kabla ya hujaumbwa kimwili ulishaumbwa kiroho, yani kwa Namna nyingine hata kabla  hujazaliwa kuna mfumo fulani wa kimaisha Mungu alikupangia wewe kuishi..

Itaendele wakati mwingine
Ubarikiwe

Mwl Judith Mbilinyi

Mawasiliano:
Facebook | | Instagram | YouTube
Email: judithmbilinyi@gmail.com
Tel: +255 762 372 408,  +255 712 657 950


Previous
Next Post »