UMEUMBWA KWA KUSUDI SHEHEMU YA 3

Namshukuru Yesu kwa Neema yake. Leo tunaendele na somo hili ..
Kuna aina mbili za uumbaji Mungu alizifanya
  1:uumbaji wa mwanadamu kiroho(spiritual)
  2:uumbaji wa mwanadamu kimwili(physically)

1: #uumbaji_kiroho (spiritual)

Mwanzo 1:26. "Mungu akasema na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu, #wakatawale ....."

Katika huu mstari kuna siri kubwa sana, Mungu anapotoa mpango (plan) ya kumuumba mwanadamu anaonesha umoja " #natumfanye_mtu sio na #tuwafanye_watu  , anaonesha umoja, lakini anapofika kwenye kugawa madaraka anasema #wakatawale , Plan inaonesha umoja lakini kwenye umiliki inaonesha wingi, Je unadhani ni kwanini? Mungu hakuwa na mpango wa kumuumba Adamu peke yake ila aliplan kumuumba na mwanamke pia, kwahiyo mwanamke na mwanaume wote walishaumbwa katika ulimwengu wa Roho kabla ya kuumbwa katika ulimwengu wa mwili.

  Mwanzo 1:27 "Mungu akaumba mtu kwa mfano wake , kwa mfano wa Mungu alimuumba Mwanamume na mwanamke"

Kwahiyo suala la mwanamke kuumbwa halikuwa Plan B, hapana, mwanamke na mwanamume wote waliumbwa katika ulimwengu wa Roho kwa kusudi, na sio kwamba mwanamke aliumbwa baada ya mwanamume , hapana, Kumbuka hapa tupo katika uumbaji katika ulimwengu wa Roho, tupo katika mpango (plan)ambayo Mungu alikuwa akiplan juu ya mtu, lakini Huyo mtu alikuwa bado hajadhihirika kimwili kama mwanadamu, kwa upande mwingine naweza sema Mungu alikuwa anamuumba mtu Roho kabla ya ya mtu mwili (mwanadamu),

  2:#uumbaji_kimwili (physical)

 ukisoma katika Mwanzo 2:7
     "Bwana Mungu akamfanyia mtu kwa mavumbi ya Ardhi , akampuulizia puani Pumzi ya uhai, mtu akawa Nafsi hai"

Hapa tunaona uumbaji wa Mungu kimwili, Baada ya kumuumba mtu Roho, kisha anakuja kumuumba mtu mwili, na hapa tunaona bado uumbaji unaonesha umoja #akamfanya_mtu" sio watu, lakini katika Mwanzo 1:26 tumeona kuwa alimuumba mwanamke na Mwanamume, lakini katika uumbaji kimwili anaonesha kumfanya mtu na sio watu, kwanza ni lazima ujue utofauti wa maneno haya ,

#Akasema_na_tumfanye Mwanzo 1:26 na katika Mwanzo 2:7 inasema #Bwana_Mungu_akamfanya_mtu...
Akasema na tumfanye inaonesha kama plan (mpango Fulani) lakini katika Mwanzo 2:7 inaonesha uthibitisho wa ule mpango au plan ya Mwanzo 1:26, kwa namna nyingine tunaweza kusema katika Mwanzo 1:26 inaelezea uumbaji wa mtu kiroho lakini katika  Mwanzo 2:7 inaonesha uumbaji wa mtu (roho+nafsi)+ nafsi =mwanadamu

đź“Śsasa katika ulimwengu wa Roho Mungu alimuumba mwanamke na mwanamume , lakini katika ulimwengu wa mwili Mungu alianza kumfanya mwanamume kwanza na kisha mwanamke

👉suala la wewe kuwa mwanamke au mwanamume halizuii kuliishia kusudi , hata siku moja usijilaumu kwanini ulizaliwa mwanamke au mwanamume sababu jinsia haina chochochote cha kufanya juu ya wito au kusudi uliloitiwa

👉mwanamke kuumbwa baada ya Adamu haina maana kuwa yupo chini ya mwanamume  na kwamba hana uwezo wa kufanya maamuzi ila ilikuwa mpango tu wa Mungu kuwa mwanamke atoke ubavuni kwa Adamu .. Tumeona kuwa katika ulimwengu wa Roho Mungu alimuumba mwanamke na mwanamume lakini katika kuwadhihirisha katika ulimwengu wa mwili alitumia njia hizo kumdhihirisha

Angalizo
Biblia inasema mume ni kichwa cha familia na mwanamke anatakiwa kumheshimu mume wake lakini sio kufanyika mtumwa.
Mara nyingi jamii  hapo zamani  imekuwa ikiwaweka wanawake chini na kuona kama hawana nguvu  ya kufanya maamuzi na hata kuwazuia kuhudumu lakini ashukuriwe Mungu yeye aliyetupa Neema sasa tunaweza kusimama na kuvitumia vile vipawa alivyotupa

đź“Ślakini tusitumie nafasi hii kuwa wanaume.. I remember Dada yangu mama yangu Winnie Moses kuna kitu kikubwa alinifundisha .. Kuna wanawake wengi nowdays wanaweka jitihada kuwa wanaume,  yani physical ni wanawake lakini by actions ni wanaume.
Ni vema kila mwanamke (binti) akatambua nafsi yake na akaitumia vile ipasavyo pasipo kuvuka mipaka..
  Enyi wanawake watiini waume zenu,
  Mwanamume ni kichwa cha familia..
đź“Śkuwa kichwa cha familia haina maana kila unachosema hata kama ni pumba basi wakifate no.. Na kuwa kichwa sio tu nafasi ila na majukumu pia, ni kwa kivip unaweza kuilea familia, je matendo yako yana kuwakilisha kama kichwa? Kuwa kichwa ni majukumu na sio jina tu.

Mungu akupe kuelewa zaidi
Tutaendele wakati mwingine..
Mwl Judith Mbilinyi

Mawasiliano:
Facebook | | Instagram | YouTube
Email: judithmbilinyi@gmail.com
Tel: +255 762 372 408,  +255 712 657 950


Previous
Next Post »