Utangulizi
Ndugu Mpendwa neno Mtakatifu
ni pana sana kulifahamu, na kila MTU analijua kwa namna yake huyu hivi na huyu vile.
Lakini kwa kadri ya ufunuo ulioko ndani yangu somo hili hatuwezi kujifunza hata 1/8 ya somo kwa siku
hata kwa wiki. Kwa Leo naomba tutafakari kwa pamoja sehemu ya utangulizi tu na
ninaamini Mungu ataweka ari ndani yako ya kuendelea kujifunza zaidi juu ya somo
muhimu sana la utakatifu.
UTAKATIFU ni tabia pekee ya
Mungu inayoelezea jumla ya sifa, utendaji na uwepo wake. Hakuna tabia nyingine
ambayo ni kuu kuliko UTAKATIFU kwa Mungu wetu.
Wanadamu tunampa Mungu sifa
nyingi sana, ana upendo, ni mwema, ana huruma, ana Neema, ni mpole, ana nguvu,
ni mkuu, na nyingine nyingi sana lakini UTAKATIFU ni Sifa pekee na Tabia kuu ya
Mungu inayozaa sifa zote tumpazo Mungu.
Sifa zote tumpazo Mungu,
ibada zote tumpazo Mungu, shukrani na heshima tumpazo Mungu, zote ni kwa sababu
yeye ni Mungu Mtakatifu.
Ukisoma katika kitabu cha Isaya 6:3 “Wakaitana, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu,
Mtakatifu, ni BWANA wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake.”
Zingatia "Mtakatifu,
Mtakatifu, Mtakatifu........... Utukufu wako"
Biblia haijasema, mwema,
mwema, mwema, au mwenye upendo, mwenye upendo, mwenye upendo, wala mpole,
mpole, mpole,au mkuu, Mkuu, mkuu. Bali Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu.
Zingatia yafuatayo kabla
hatujaendelea:
ü Standard ya maisha katika ufalme wa Mungu ni
UTAKATIFU.
ü Wote watakaoingia katika ufalme wa Mungu lazima wawe
watakatifu, yaani tiketi ya kuingia mbinguni ni utakatifu.
ü Uhalali wa mwanadamu kutembea na Mungu ni UTAKATIFU.
ü Kila kitu kitumikacho kwa ajili ya Mungu lazima kiwe
kitakatifu, hata kikiwa kichafu kwa asili lazima kiwekwe wakfu kwa ajili ya
Mungu.
Soma vifungu vifuatavyo;
1 Petro
1:16 “kwa maana imeandikwa, Mtakuwa
watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.”
Waebrania
12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na
amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana
asipokuwa nao;”
Zaburi 16:3 “Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora, Hao
ndio niliopendezwa nao.”
Neno UTAKATIFU linaweza kutazamwa
katika mitazamo mingi sana.
Utakatifu kama wito. (Calling)
Utakatifu kama Viwango(Quality)
Utakatifu kama Mchakato(Process)
UTAKATIFU kama Hali(Condition)
Utakatifu kama Tukio(Event)
UTAKATIFU KAMA WITO
Mungu anapokuita anakuwa na
sababu mahususi juu yako binafsi. Na wito ni Mchakato. Wito wa Mungu mkuu kwa
wanadamu ni kuwaita wote walioridhia kuwa RAIA wa ufalme wake na warithi wa
ufalme kama wana wake wazaliwao si kwa mwili Bali kwa roho. Kwakuwa wote
wanaoitwa na Mungu huzaliwa tena kwa roho na biblia inasema kilichozaliwa kwa
mwili ni mwili na kilichozaliwa kwa roho ni roho.
Yohana 1:12-13
“Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa
kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa
damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.”
Yohana 3:6 “Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na
kilichozaliwa kwa Roho ni roho.”
Mungu anapokuita anakusudia
wewe kuwa RAIA wa ufalme wake. Mwana mteule.
Lakini kuna ‘process’
unapitia kufikia kiwango cha kuwa mtimilifu kwakuwa UTAKATIFU ni ‘process’ .
Efeso
4:11-13 “Naye alitoa wengine kuwa
mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa
wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya
huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia
umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata
kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;”
Wengi wanajua kabisa kwamba
Mungu anapokuita anahitaji ufanye kazi yake kama uchungaji, ualimu, uimbaji n.k
lakini ukweli ni kuwa hizo huduma ni Mchakato wa kulikamilisha kusudi .
Kusudi la wito
ni :
ü kuwakamilisha watakatifu
ü kazi ya huduma itendeke
ü mwili wa Kristo ujengwe.
Hivyo ili kufikia kiwango
hicho UTAKATIFU kama WITO unapitia hatua
hizi;
Ø WITO
Ø Kufanywa mwana
Ø Kupokea tabia ya baba
Ø Kuishi kwa ‘Standard’ ya ufalme
Ø Kulitumikia kusudi
Rum 8:14 “Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu,
hao ndio wana wa Mungu.”
Ili kulikamilisha kusudi LA Mungu, Utakatifu
unatakiwa uwe sehemu ya maisha yako.
‘Living Holy is achieved through kingdom standard States which involves
the Listening, Accepting and Practicing the Word of God you hear during God's
calling.
It involves your personality ie Spirit, Soul (mind,
will, emotions), Body.
- Mindsets
- Attitude
- Habits
- Character
- Living
Mindsets are maps for our living. They shape our
attitude which influences habits and behaviours that in turns describes our
character.’
Unapolisikia Neno la wito wa
Mungu lazima uwe na ‘right mindsets’ ili kukujengea ‘attitude’ itakayokupa ‘the
best habits.’
Tabia hizo ndizo zile
zinazompa Mtakatifu utukufu wake. Kanuni
ya maisha matakatifu ni kuongozwa na roho Mtakatifu. Kwakuwa hakuna maisha bila
roho hivyo maisha matakatifu bila roho Mtakatifu hayawezekani.
Kwakuwa wote wanaoongozwa na
Roho wa Mungu hao ni wana wa Mungu.
Ndugu Mpendwa katika
utangulizi huu naomba kuhitimisha kwa kusema yafuatayo:
ü Kabla ya kitu chochote unatangulia Utakatifu.
ü Mungu anatuita tukiwa waovu ili tuwe watakatifu.
ü Kabla ya huduma yako Mungu anataka UTAKATIFU kwanza.
ü Kabla ya maisha yako Mungu anataka UTAKATIFU kwanza
ü Kabla ya mafanikio yako Mungu anataka UTAKATIFU
Kwanini?
Kwa sababu kwa UTAKATIFU wake
dunia yote inajaa utukufu wake na aliahidi utukufu wake hatampa mtu mwingine Isaya 42:8 Mimi ni BWANA; ndilo jina
langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu.
Katika ufalme wa Mungu ulio
katika asili ya UTAKATIFU tunatafuta usahihi wa vitu kabla ya kuvifanya kwa
usahihi. ‘Doing right things before doing things right.’ Mungu hataki umtumikie Bali anataka utumikie kusudi lake
sahihi Kumbuka ‘Abuse is inevitable if the Right purpose is unknown.’
Utakatifu sio ule tu unaoonekana kwa nje Bali hata ule
wa ndani usioonekana. Mambo Yale unayoyafanya ukiwa mwenyewe, chumbani
kwako au popote pa siri, Mungu anayachunguza Sana. Na anayemheshimu Mungu Toka
sirini Mungu anamheshimu sana.
UTAKATIFU sio cheo, wala kitu cha kusomea,
wapo wanaoamini kuwa kusoma bible school, kuwa Mchungaji, askofu, padre sister
kwamba ndo UTAKATIFU sio kweli . UTAKATIFU ni wito wa Mungu.
UTAKATIFU sio wa rika Fulani. Wapo wasemao
Vijana hawawezi kuwa watakatifu, kwani vishawishi ni vingi, wengine wanasema
mimi nitakuwa Mtakatifu nikioa au kuolewa, au nikizeeka. Huko ni kujidanganya mwenyewe.
Utakatifu ni wa kila mtu na
ni hapa duniani. Wapo wasemao hakuna watakatifu duniani hayo ni mawazo ya
kibinadamu kwani Mungu mwenyewe kasema anapendezwa na watakatifu walioko
duniani.
Tabia hizi ni lazima
kwa kila Mtakatifu:
Kusoma neno na kuliishi.
Kuomba kila siku
Kuongozwa na Roho Mtakatifu,
Kulitumikia kusudi sahihi na
Kujitoa kwa Mungu kwa hali na mali
“Hata
wewe una haki ya kuwa mtakatifu, kama tu utakubali wito na kukubali kuishi
katika kusudi la Mungu.”
‘To experience holy life is
hard But Not Living holy is harder.
In order to live a life you
never lived before you need to pay a cost you never paid before and acquire
knowledge you never acquired before.’
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon