Ukweli ni kwamba hakuna siku ulimwengu utakupa muda kufocus na mambo ya Mungu. Ulimwengu unachofanya ni kukuweka busy na kukuonesha kwamba unawajibika kwa mambo mengi. Ukikaa ukiyachunguza waweza kukuta 95% ya muda iko katika kukidhi mahitaji ya mwili.
Endapo tutakwama kung'amua hili, taratibu litatafuna Roho zetu, kwasababu tutawekeza sana mwilini na kusahau Rohoni.
Rai yangu si kwamba tupuuze kufanya majukumu yakukidhi mwili, ila ni kwamba katikati ya hayo majumu mengi tutengeneze Muda na Baba. Usiwe Muda wa ziada, lakini upewe kipaumbele kama yanavyopewa mambo mengine.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon