UNYENYEKEVU ✍🏻📚
Moja ya madarasa ambayo huenda yakakupelekea kujiona kama unaonewa, huheshimiwi, huthaminiwi ni dasara la unyenyekevu. Kubali mchakato katika kuvunjwavunjwa kiburi hata kama ni katika wingi wa maumivu. Unyenyekevu haupimwi kwa kuheshimika, kuthaminiwa , bali kutoheshimika, kutothaminiwa, Katika wingi wa dharau na maonezi. Kunyenyekea kunahitaji nguvu kubwa kuliko kujikweza. Wenye nguvu hunyenyekea, watu dhaifu hujikweza. Kuwa na ufahamu ni jambo la kwanza, lakini ili ufahamu uwe tabia unahitaji mazoezi. Wewe ni yule yule mpaka utakapokua kile unachokifahamu
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon