kinachofanya shetani apambane na wewe katika maisha yako sio kwasababu ulizaliwa katika hali ya umasikini wala sio kwasababu hauna wazazi wala sio kwasababu ya umri ulionao ila ni kusudi ulilolibeba.. Shetani hapambani nawewe kwasababu una umri mkubwa au mdogo... Hapambani nawewe kwasababu wewe ni tajiri au masikini anapambana nawewe kwasababu ya kusudi ulilolibeba... Ulipozaliwa mbingu zilijua kusudi uliloitiwa na kuzimu(shetani) pia ilitambua kusudi ililoitiwa Isaya 58:8 .. Kwahiyo shetani anapopambana nawewe tagert yake kubwa sio wewe ila ni kusudi ulilolibeba na ndio maana kuna majaribu unayapitia wewe lakini wengine hawayapitii.. Kuna ugumu unaupitia wewe lakini wengine hawaupiti..
Jaribu lako ni tofauti na lá rafiki yako sababu kila mmoja amebeba kusudi tofauti tofauti na shetani anapopambana Na wewe kupitia majaribu usitegemee kuwa ataachilia jaribu linalofanana Na mwingine.. Na ndio maana Yesu alisema yoyote anayetaka kunifata sharti ajikane, ajitwike msalaba wake kisha anifute. Sio ajitwike na msalaba wa rafiki yake.. Ukisoma Yeremia 1:5-10 utaona jinsi Yeremia alipokuwa akiambiwa na Mungu juu ya kusudi ambalo Mungu amemuitia... Ule mstari wa tano "Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, Na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa, Nimekuweka kuwa nabii wa mataifa" Maisha ya mwanadamu yamebebwa na kusudi. Kinacholinda uhai wako sio tu umri ulionao ila ni kusudi..( Naupenda wimbo wa Paul clement unasema uhai huu unalindwa Na kusudi lako) .. Kuna maeneo Mungu amekupitisha ambayo kwa hali yakibinadamu yalikuwa magumu kupita lakini kwasababu tu ya kusudi ulilolibeba ulipita salama, kuna ajali Mungu amekuepusha sio kwasababu wewe unastahili sana ila ni kwasababu ya kusudi ulilolibeba, Ester aliingia kwa mfalme kinyume cha taratibu na hakuhukumiwa, kilichomlinda sio umalkia aliokuwa nao ila ni kusudi alilokuwa amelibeba, shetani tagert yake kubwa anapombana na wewe ni kuharibu kusudi ulilolibeba sababu anajua kuwa kusudi ndilo limebeba mfumo mzima wa maisha yako. Na ukilijua hili litakusaidia hata namna ya kuomba.. Maadui wakija kwako hutawaona kwa namna ya kibinadam ila utawaona zaidi ya kibinadamu (beyond) . Hii itakusaidia kujua piá kwanini majaribu unayoyapitia wengine hawayapitii.. Kinachowatofautisha ni kusudi mlilolibeba na ujue ya kuwa kama kila mtu ameitwa kwa kusudi tofauti basi hata namna mashambulizi itakayotumika kuliua kusudi ni tofauti.. 👉shetani haoni shida kuangamiza maelfu ya watu ili apate kumuangamiza mbeba kusudi wa Mungu.. Kuna ajali nyingine huwa zinatokea na kiuhalisia zililenga kukuangamiza wewe na wengi wakafariki katika ajali hizo lakini Mungi akakupigania ukatoka salama .inawezekana hujanielewa .ngoja nirudie kwa mfumo huu.. Ukisoma mathayo 2:1-23 utaona habari zakuzaliwa kwa Yesu.. Yesu alipozaliwa Herode alipata shida Na alihisi kuwa Yesu amezaliwa kumnyang'anya madaraka na kumbe Yesu hakuja kwa namna hiyo.. Unaweza kujiuliza maswali machache. Herode pamoja Na ukubwa wake lakini bado ilimpa shida pale aliposikia Yesu amezaliwa ambaye bado alikuwa ni mtoto mchanga na hata kama angekuwa amekuja kumiliki kwa mifumo ya kidunia bado kwa kipindi kile umri wa Yesu ulikuwa hauruhusu.. Alafu Herode kawatuma mama Jusi wakienda warudi kumpa habari nayeye aende kumsujudia, na alipoona hawajarudi akatoa amri ya watoto wa kiume kuanzia miaka miwili kushuka chini wauwawe mathayo 2:16-17 lengo lake lilikuwa ni kumwangamiza Yesu sababu alijua kusudi alilolibeba ijapo hakufanikiwa kumwangamiza Yesu.. Jifunze pia kwa Musa kutoka 1:1-22 Utaona jinsi maisha yake yalivyokuwa yamesongwa na majaribu.. Alipozaliwa Tu musa mfalme alitoa amri yawatotó wakiebrania kuuwawa.. Sasa unaweza kujiuliza kwanini kauli hii ilitoka baada yakuzaliwa kwa Musa au Yesu.. Unapozaliwa mbingu na kuzimu na maadui hujua kusudi la kuzaliwa kwako na ndio maana hutumia njia mbalimbali kukuangamiza lengo Tu ni kuuwa kusudi ulilolibeba.. Kuna mambo unayapitia sio kwasababu ya asili yako ila ni kwasababu ya kusudi ulilolibeba, pia shetani yupo radhi kuangamiza kundi kubwa la watu ila Tu ampate mwenye haki Mmoja wa Mungu. Najua kipindi cha herode kuna watotó wengi wakiume waliuwawa ambao hawakuwa Na hatia lakini aliyekuwa tagerted Ni Yesu. Lakini tunalotumaini Moja ya kuwa katika mambo yote tunashinda na zaidi ya kushinda.. Mungu akiwa upande wetu ni nani aliye juu yetu? Yesu ni ngome imara tumeikimbilia hiyo Na hatutatikisika Kamwe. Yesu akusaidie katika ugumu wowote unaoonekana mbele yako.. Yesu akufanyie wepesi.. Akusaidie kuvuka salama na maadui wasikushinde Ubarikiwe judithmbilinyi@gmail.com 0762372408
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon