​​​NENO LA IMANI YA KWELI​​​

​Albert Ochieng​✍🏼


Warumi 10:17
​​​Basi Imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.​​​

​​​Imani yoyote huja kwa kuskia neno lolote,​​​ mwanzoni tulizoea kuskia neno la dunia hii kupitia wazazi na jamii. Maneno hayo yakabumba Imani iletayo hofu, Shaka, woga, mauti, dhambi. Mungu akaachia Neno la ​KWELI​ ili ​TUCHUJE​ ya ​UONGO​ yaani ya dunia hii. Ili mradi tupate Imani isiyo na mawaa, isiyoleta hofu wala kupelekea mauti.

​​​Ili kuondoa soda ndani ya glass na kupata maji. Kinga glass bombani kadili maji yanavyo ingia ndivyo soda humwagika na kubaki maji tupu.​​​ Vivyo hivyo ruhusu ​NENO​ kujaa moyoni mwako na kuliweka kwenye matendo, huko ndiko kuukulia wokovu yani ukweli kuhusu wewe. Kwani tumezaliwa upya hatuna budi kujilisha na kulishwa hata tukue katika ​UKWELI​.

​​​Watumie wengine wengi hata tufike miisho ya dunia.​​​🌍

Contact: 0753812881
Insta- Albert_ochieng
Previous
Next Post »