🍃Maandiko yana tuambia kwamba *watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa*. Watu wanaangamia si kwamba hawajui vitu hapana, wanajua vitu lakini wanapotoshwa. Ule ukweli unaoujua unapindishwa kiulaini, na kwa dunia ya leo imekuwa ni kawaida sana. Watu wanaifanya dhambi ionekane kitu fulani kizuri ambacho unafikiri ukikikosa itakuwa kidogo shida. Kumbe sivyo. Na maandiko yalitahadharisha kuhusu hilo _*shika sana ulichonacho asije mwovu akakunyang'anya*_
🍃```Adam na Eva```
Kukosa utii kwa Adam na Eva ilikuwa siyo kwamba hawakujua. Walijua kabisa Mungu amekataza tusile tunda kwenye mti wa katikati na tukila tu tutakufa. Lakini angalia janja ya Ibilisi, anawadanganya kwamba Mungu hatakimjue vitu vingi, mkila matunda mtakuwa kama yeye (Mungu).
🍃Shetani anataka *wakose kutii*, anajua anawadanganya lakini anatumia njia ya kufanya lile tunda kuvutia zaidi.
```Swahili Union Version MWA. 2:16-17 BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.```
```Swahili Union Version MWA. 3:1-6 Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani? Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula; lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa. Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya. Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.```
_Mara nyingi tumekosa kumsikiliza Mungu tu kwasababu, wapo watu ambao tunawafikilia watatuonaje. Watu wengi hasa vijana wamekuwa ni sababu ya kukosesha wenzao kumtii na kumsikiliza Mungu na hatimaye kupelekea maumivu makubwa katika maisha._
```Ee Mwenyezi Mungu, tujalie nguvu ya kumshinda adui anaifanya dhambi kuwa kawaida tu mbele za macho yetu. Tule macho ya rohoni tuweze kuona kusudi la wito wetu ili tuendelee tukutii na kulifuata neno lako. ```
Amen.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon