UTII 1

Na Wicklif Benjamin 

🍃Kutii ni kuheshimu mamlaka zilizowekwa. Ni kufuata sheria kilizowekwa bila kushurutishwa na mtu yeyote. Huweza kutokea kwa matakwa ya mtu (voluntary obedience) au ukatokea pasipo kutaka (involuntary obedience).

🍃Kwasababu Mungu alipo mwumba mwanadamu alimpa akili na utashi wa kufanya na kuamua mambo, basi huwa anataka na anakubali ule utii wa utashi (voluntary obedience). Ndiyo maana anataka watu wapate maarifa, hekima na ufahamu, ili wanapoamua mambo wafanye kwa utashi wao wenyewe.

Hes. 27:12-23
_Yoshua anafanywa kiongozi baada ya Musa. Mungu anamwambia Musa aweke sehemu ya heshima yake mbele ya makutano ya Israeli ili watii._

Kwanini Mungu anamwagiza Musa kufanya hivi mbele ya mkutano wa waisraeli? Ni ili wajue ya kwamba Yoshua ataongoza badala ya Musa hivyo kwa *utashi wao wenyewe* waweze kumtii.

```Ee mwenyezi Mungu, tujalie neema ya kukujua zaidi, tuwezeshe kukutii na kuyafanya mapenzi yako. ```

Amen.
Previous
Next Post »