Msamaha

RAFIKI YANGU MPENZI
Na Goodluck Ernest 
Marafiki wawili walikuwa wanatembea jangwani. Wakiwa safarini ukatokea ubishani kati yao na mmoja kati ya marafiki wale akampiga kibao cha usoni mwenzake.

Yule ambaye alipigwa kibao aliumia na bila kusema kingine chochote akainama chini na kuandika katika mchanga: LEO, RAFIKI YANGU MPENZI AMENIPIGA KIBAO CHA USO.

Baada ya hapo wakaendelea kutembea, hadi walipokutana na chemichemi katika jangwa. Na hapo wakaamua kuoga na ndipo yule ambaye alipigwa kibao mwanzo wa safari yao akazidiwa na maji na kuanza kuzama lakini rafiki yake akaenda kumuokoa.

Baada ya kuokolewa kutoka katika kuzama, akaandika katika jiwe: LEO, RAFIKI YANGU MPENZI AMEOKOA MAISHA YANGU.

Ndipo yule rafiki aliyempiga kibao na kumuokoa rafiki yake akauliza, "Baada ya kukuumiza uliandika katika mchanga na sasa umeandika katika jiwe, kwa nini?"

Rafiki akajibu, "Pale mtu mwingine anapotuumiza, yatupasa tuandike chini katika mchanga ambapo upepo wa msamaha waweza kufuta. Lakini pale mtu mwingine anapotufanyia jambo zuri, ni lazima tuandike katika jiwe ambapo hakuna upepo wowote utakaoweza kufuta. (Annony..)

Kumbuka: Haijalishi huyo rafiki yako ni mzuri kiasi gani bado ni mwanadamu, kuna siku atakuumiza na ni lazima umsamehe kwa hilo.

Tukutane Alhamisi ijayo....

#SAMEHE, ISHI SALAMA

Goodluck Ernest, The Diplomat
+255 713 660921
mashambo.ge@gmail.com
Previous
Next Post »