UMEUMBWA KWA KUSUDI SEHEMU YA 2

Katika somo lililopita tulijifunza maana ya kusudi na uumbaji wa Mungu lakini Leo natamani tuangalie kitu kingine..
Na Judith Mbilinyi 

KWA NAMNA GANI TUNAFANANA NA MUNGU

Mwanzo 1;26 " *Mungu akasema* , Na tumfanye mtu kwa *mfano_wetu*, kwa *sura_yetu*....."

"Mungu akasema" hii inaonesha kwamba ilikua ni plan, ni mpango ambao bado haujaanzwa kutekelezwa, ni wazo, na wazo ni kitu kilichopo katika ulimwengu wa Roho ,

  "Na tumfanye mtu kwa Mfano wetu, kwa sura yetu..."
Kumbe tunafanana na Mungu kwa utu wetu, Mungu alituumba sisi kwa mfano wake , kwa sura yake, yani tunafanana  na Mungu, watu wanapotuona sisi wanatakiwa kumuona Mungu aliyepo ndani yetu, na hii ilithibitisha ni kwa kiasi gani Mungu alimuheshimu mwanadamu, ukisoma utaona hakuna kitu chochote kilichoumbwa kwa mfano wa Mungu ila ni mtu tu.
Sasa unaweza  kujiuliza kwamba ikiwa tumeumbwa kwa mfano wa Mungu Na sura ya Mungu sasa mbona kila mtu anasura yake, sikia sisi wanadamu tunafanana na Mungu kwa utu wetu kwasababu mtu ni muunganiko wa Roho na nafsi na mwanadamu ni muunganiko wa Roho ,nafsi na mwili, Mungu anayo nafsi na Roho pia lakini hana mwili, kwahiyo tunafanana na Mungu kwa utu wetu na sio kwa miili sababu Mungu hana mwili na ndo maana  hata Yesu alipokuja duniani ilimlazimu azaliwe na mwanamke ili awe mwanadamu kama sisi Ijapo yeye alikuwa ni Mungu.

Mwanzo 1:26  "Mungu akasema  Na tumfanye mtu kwa mfano wetu ,kwa sura yetu , *Wakatawale* samaki....."

Unaweza kujiuliza kwamba kwanini Mungu alisema na *tumfanye* na kwanini hakusema *Nanimfanye* mtu? , Naamini tunajua tunapomzungumzia Mungu , Mungu ni mmoja ambaye yupo kwa namna tatu, au anajidhihirisha kwa namna tatu, Mungu baba , Mungu mwana, na Mungu Roho mtakatifu na ndio maana hapo alitumia wingi, mwanadamu yoyote yule ana Nafsi na  ana Roho  na  hiyo inamkamilisha kuwa mtu, lakini ongezeko La mwili linamfanya kuwa mwanadamu , mtu yoyote alieyeokoka Mungu hufanya makao ndani yake kwa upande mwingine Mungu baba, mwana na Roho mtakatifu hufanya makao ndani yake, na watu wanapomuona Huyo mtu hawawezi kumuona yeye ila watamuona Mungu aliye ndani yake sababu Mungu yupo ndani yake na wewe ndani yake , Na hapo ndipo like andiko la "tumfanye mtu kwa mfano wetu na kwa sura yetu, wakatawale...." Linapotimia

Tutaendelea wakati mwingine.
MUNGU AKUBARIKI

Mwl Judith Mbilinyi

Mawasiliano:
Facebook | | Instagram | YouTube
Email: judithmbilinyi@gmail.com
Tel: +255 762 372 408,  +255 712 657 950


Previous
Next Post »