Moja ya vitu ambavyo vinawasumbua wakristo kuvielewa ni kitu ambacho kimefanyika msalabani. Leo nitaongelea sehemu moja ya kilichofanyika msalabani.
~Kuimaliza dhambi na nguvu yake na kuiondoa dhambi kabisa
Kuna ufahamu umezoeleka kwamba dhambi zetu zimefunikwa kwa damu ya Yesu, kwa ujasiri wote nataka nikwambie si kweli! Its wrong! Our sins are washed away.
Yohana mbatizaji alipomuona Yesu alipata ufunuo wa ajabu kuhusu Yesu
Yohana 1:29
"...Tazama mwanakondoo wa Mungu Aichukuaye dhambi ya ulimwengu.."
Ukisoma biblia ya kiingereza inasema
"..behold the Lamb of God who takes away the sins of the world"
Mpendwa ndani ya Yesu Kristo kupitia msalaba si kwamba dhambi zetu zimefunikwa au tumesamehewa nusu nusu. Dhambi zetu zimeoshwa, kusamehewa na kuondolewa zote.
Si kwamba dhambi zako zinasamehewa Jumapili baada ya Jumapili, ama kutoka kosa baada ya kosa! Hapana! Dhambi zako zimesamehewa na kuoshwa mara moja tena moja kwa moja (Your sins were washed away once for all.)
Wengi tunashindwa kuelewa kuwa msalaba umechukua dhambi na kuzifuta, za sasa, zilizopita na zijazo, hakuna rekodi ya dhambi kwa mtu aliye ndani ya Kristo Yesu.
Warumi 4:8
Heri mtu yule ambaye Bwana hamhesabii dhambi.
Mungu ana uhalali wa kutokukuhesabia dhambi sababu aliiadhibu dhambi katika mwili wa mwanae Yesu Kristo msalabani.
2 Wakorintho 5:21
Yeye Asiyejua dhambi, alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa Haki ya Mungu katika Yeye.
Ukweli ni kwamba kulikuwa na mabadilishano msalabani. Yesu alifanyika kuwa dhambi nasi tukafanyika kuwa Haki. Hii ilifanyika mara moja tu. Yesu hafanyiki mara nyingi nyingi kuwa dhambi, hatakufa tena. Alikufa mara moja tu. Hio inamaanisha hata sisi tunafanyika mara moja tu kuwa Haki ya Mungu.
~Je, dhambi si dhambi kwa kiumbe kipya?
Mtu aliye ndani ya Kristo, ukweli ni kwamba, akifanya tendo la dhambi litaendelea kuwa la dhambi tu. Dhambi ni dhambi. Kuna uchaguzi, kwenda sambamba na upya na haki tuliyonayo katika Kristo ama kuufuata mwili na kutenda dhambi.
~Je, kukosea kwa mwenye Haki kunaondoa Haki yake ndani ya Kristo?
Kukosea kwa aliye ndani ya Kristo kupo. Wengi wetu tumekosea na nieleweke kuwa dhambi ni dhambi. Lakini kukosea kwa kiumbe kipya hakubadilishi haki aliyonayo ndani ya Yesu.
Alichokifanya Adam hakikufutika kwa matendo na alichofanya Yesu kamwe hakiwezi kufutika kwa matendo kwetu sisi tuliomwamini.
~Ukigundua umekosea ufanye nini?
Stop! Acha, fanya vitu vinavyoenda sawa na asili yako mpya, uliumbwa utende yaliyo mema.
Kugeuka na kuifuata asili yako kiumbe kipya, ndio toba ya kweli. Ukweli ni kwamba tukikosea tunatubu si ili tusamehewe. Tunatubu kwasababu Yesu kupitia msalaba, ameshatusamehe.
Mtu aliye nje ya Kristo hawezi kutubu, atubu aelekee wapi? Hana direction, amekufa! Abadilishe fikra (toba) kumuelekea nani?!
Hakuna toba kwa aliye nje ya Kristo. Unaweza kusema kuokoka lakini kuokoka sio toba, ni kuzaliwa upya (tuache hii iko katika series ya 2😊)
~Je, tufanye dhambi sababu tumeoshwa dhambi zote na Mungu anatuona kama viumbe vipya?
😳 Thats stupidity
Hutakuwa na furaha kamwe ukienda kinyume na asili yako na unampa uhalali shetani kupata njia za kukutesa.
Warumi 6:16
Ukweli unabaki kuwa palepale, dhambi na nguvu yake ilimalizwa yote msalabani. Yesu alikufa na kulipa dhambi zetu zote na tulipookoka Roho zetu zilifanywa upya kabisa, biblia inasema roho zetu zikawa sealed na Roho Mtakatifu.
Napenda biblia ya kiingereza inavyosema;
In whom ye also trusted, after that ye heard the word of truth, the gospel of your salvation: in whom also after that ye believed, ye were sealed with that holy Spirit of promise, Ephesians 1:13
Ulipookoka si kwamba tu rohoni ulizaliwa upya, roho yako ilikuwa sealed na Roho Mtakatifu..
Your spirit is holy and perfect na mpaka Yesu anakuja, dhambi na vitu vyovyote vichafu haviwezi kupenya rohoni mwako sababu Roho Mtakatifu ameweka muhuri, ame seal kisawasawa.
Dhambi inaweza kuathiri mwili na nafsi, ila si roho, Rohoni mwako mara zote kutakuwa salama.
Na Mungu huhusiana nasi katika Roho, Mungu ni Roho. Hivyo uliye ndani ya Kristo, uliyezaliwa upya, haiwezekani Mungu kukuona tofauti ikiwa uko sealed na Roho Mtakatifu.
Ndio maana Mungu alikuwa na ujasiri wote kumwambia late Tr Kenneth Hagin kuwa anamrudisha William Branham mtumishi wake nyumbani kwa kufundisha doctrine mbaya. Swali la kujiuliza ni je, William Branham hakukosea? Alikosea na Mungu alijua makosa yake na jinsi yanavyoweza kuligharimu kanisa, ila akaamua kumrudisha nyumbani, kwanini?
Ephesians 1:13 ilikuwa alive kwake, in his spirit alikuwa amekuwa sealed na Roho Mtakatifu. He was perfect and holy bado.
~Je, matendo ya utakatifu si muhimu??!
Ni muhimu sana. Hutampa shetani nafasi ukiishi kwa utakatifu wa matendo, hutaleta magomvi na mafakarano. Naichukia dhambi kwa inachofanya, inaharibu familia, mahusiano na miili. Ingawa kwa Mungu, utakatifu ni zaidi ya matendo. Ni kuwa ndani ya Yesu Kristo, kiumbe kipya.
Kiumbe kipya hana past na future yake iko kwa Mungu pekee.
~Je, ukishakuwa kiumbe kipya kuna uwezekano wa kubadilika na kuwa kiumbe cha zamani?! Haiwezekani! Hata dhambi haiwezi kukubadilisha kuwa kiumbe cha zamani. Dhambi imelipiwa tayari.
Kuzimu watakwenda waliokataa provision ya dhambi, Yesu Kristo. Ukweli ni kuwa Yesu aliiharibu dhambi msalabani. Dhambi haina nguvu kwa aliye ndani ya Kristo na hata ikatokea ukitenda kosa, inuka knowing that you are free from sin na matokeo yake.
Hutakuwa huru kweli kweli mpaka ujue sasa hakuna nguvu ya dhambi kwa aliye ndani ya Kristo. Dhambi na madhara yake havina nguvu juu yako, wewe ni Haki ya Mungu.
Itaendelea..
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon