Waabuduo halisi

Na Judith Mbilinyi 

Kumwabudu Mungu au kumsifu Mungu ni zaidi ya kuimba, Ni zaidi ya kuimba taratibu au harakaharaka,  neno kuabudu linatokana na ibada..kitendo cha kufanya ibada ni kuabudu..
Mara nyingi tumejenga mtazamo kuwa kusifu na kumwabudu Mungu ni kupitia uimbaji tu, lakini Leo natamani kukwambia kuwa kumwabudu na kumsifu Mungu ni zaidi ya kuimba, yani kwa upande mwingine uimbaji ni moja kati ya njia nyingi za kumwabudu na kumsifu Mungu.

           Image result for worship image.png
 Maisha yetu ya kila siku yana nafasi kubwa sana katika kumwabudu Mungu, jinsi tunavyoishi, jinsi tunavyowajibu wengine , maneno yetu,miendendo yetu yote yaweza kumwabudu Mungu, Tunaposema  true worshiper is a life style, maana yake wewe kama ni mwabudu halisi basi  tunategemea mfumo wako mzima wa maisha utabebwa na ibada, yani tukikuona mtaani ndivyo tulivyokuona kanisan, sababu hatujaitwa kumwakilisha kristo madhabahuni tu kisha tukiwa mtaani tunakuwa watu wengine, no hilo sio kusudi tuliloitiwa, kwa matendo yako watu watajua kuwa Wewe ni muabudu halisi au muigizaj, Kilichowafanya wale waliomsulubisha Yesu kumhisi kuwa Petro ni mmoja wa wanafunzi wa Yesu ni jinsi Petro alipokuwa akiongea na jinsi alivyokuwa akitembea kuliwafanya watu kuhisi kuwa naye ni mmoja wa wawafuasi wa Yesu, Matendo yetu yanahubiri sana kuliko tunavyoweza fikiri,.. MUNGU ANATAMANI TUWE WAABUDU HALISI SIO KWA VINYWA TU ILA KWA MIOYO YETU PIA,
MUNGU AKUSAIDIE KUWA MUABUDU HALISI..
UBARIKIWE
Waweza kunifollow fb kwa kujifunza zaidi👇👇

judithmbilinyi@gmail.com
0762372408


Previous
Next Post »