Ezekieli:18.24
Bali mwenye haki atakapoghairi, na kuiacha haki yake, na kutenda uovu, na kufanya machukizo yote kama yale afanyayo mtu mwovu, je, ataishi? Katika matendo yake yote ya haki aliyoyatenda halitakumbukwa hata mojawapo. Katika kosa lile alilolikosa, naam, katika dhambi yake aliyoitenda, atakufa.
Ezekieli:18.32
Maana mimi sikufurahii kufa kwake afaye, asema Bwana MUNGU; basi ghairini, mkaishi.
INAUMA SANA MPENDWA
Yaan
๐umekaa kwenye WOKOVU miaka na miaka,
๐umefunga vya kutosha,
๐umejitesa mwili wako kwa kwenda huku huko kwaajili ya injili,
๐sadaka za kutosha
๐ umeimba hadi koo kukauka,
๐umefunga alimanusura kuumwa vidonda vya tumbo
๐ฅ Alafu mwisho wa siku kwa KOSA dogo tu unaambiwa *~hayo yote yamefutwa na hayakumbukwi~*
๐ข๐ข๐ข Kinachouma zaidi ni pale utakapoona uliezoea kupishana nae akijiendea kwenye mambo ya *~ANASA, STAREHE NA YASIFOA HATA KIDOGO~* *MNAPISHANA ANAINGIA KWENYE LANGO LA KULIA ALAFU WE UNAELEKEZWA LANGO LA KUSHOTO*
๐๐๐ hakika itauma sana lakini ndo ishakua hivo
๐๐๐ utatamani siku zirudi nyuma *UREKABISHE* ulipo *HARIBU* lakini nafasi hiyo ndo tiyari itakua kama upepo uliokwisha kupita hauwezi kurudi tena
Mpendwa wakati sio wakati wa kulala umefumba macho maana hujuhi ni wakati gani vazi lako litatiwa DOA
MUHIMU:
Hakikisha kila wakati unatubu na kujitakasa maana zipo DHAMBI MFICHO ambazo kwako yawezekana usizidhanie kuwa ni dhambi, ila mwisho WA siku zikakuponza
Bwana awe nawe mpedwa
Ni hayo TU niliyohitaji kukumbusha
Blessed much brethren
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon