JIFUNZE KWA YAKOBO

Na Denis Mushi

Moja kati ya watu ambao Biblia inawazungumzia Kwa sehemu ni Pamoja na Yakobo (Israeli)... katika mambo ambayo ambayo Biblia inamzungumzia yapo mengi ya kujifunza Leo natamani tushirikishane baadhi ya vitu Roho mtakatifu alikuwa akinifundisha juu ya YAKOBO
Kuna vitu vingi ambavyo naweza kukushirikisha kutoka Kwa Huyu Yakobo ambavyo ukivitafakari Kwa kina lazima upate ufahamu mpya....
Labda tuangalie baadhi ya sehemu za kujifunza kutoka Kwa Yusufu
*1:ENEO LA KIUCHUMI*
*2:ENEO LA KIMAHUSIANO (RELATIONSHIP)*
*3:UHUSIANO WAKE BINAFSI NA MUNGU*

Naomba nianze na sehemu hii ya tatu👇🏻👇🏻
UHUSIANO WAKE NA MUNGU 👇🏻
Katika vitu ambavyo Yakobo alifanya tuanze kujifunza ni hili eneo la UHUSIANO WAKE NA MUNGU....
Yakobo amekuwa akinivutia mno namna ambavyo alianza kutengeneza uhusiano wake na Mungu
Ukiangalia vizuri Familia aliyotoka Yakobo ilikuwa ni familia iliyokuwa na Agano na Mungu Kwa lugha Ya sasa tunaweza kusema ni familia ya watu waliookoka.
Kule kuwa ametoka kwenye familia inayomjua Mungu hapakumfanya Yakobo asiwe na kiu ya kumtafuta Mungu na kutengeneza uhusiano wake Binafsi na Mungu.
Naomba tuangalie hii mistari MWANZO 28:13
Na tazama BWANA amesimama juu yake akasema mimi ni Bwana Mungu Wa Ibrahim baba yako na Mungu Wa Isaka.......
Mungu anajitambulisha Kwa Yakobo kama Mungu Wa Baba zake Ibrahim na Isaka hatuoni akisema mimi ni Mungu wako(Yakobo)
Tuone na mstari Wa 15 Mungu anamwambia Yakobo kuwa Yupo pamoja na yeye na atamlinda kila aendako .. kwenye tafsiri ya kingereza inasema "I am with you and I will keep (watch over you with care,, take notice of) you wherever you may go and I will bring you back " Kwanini...Kwa sababu ya agano lililopo ndani ya familia aliyotoka
Licha ya YAKOBO kuahidiwa na Mungu kwamba atamlinda haikumfanya yeye aache kumtafuta Mungu awe Wa Kwake ndio maana kwenye mstari Wa 20na 21 Wa kitabu cha MWANZO 28 kuna maneno yenye nguvu YAKOBO ANAYOZUNGUMZA 👇🏻👇🏻
"Yakobo akaweka nadhiri akasema MUNGU AKIWA PAMOJA NAMI AKANILINDA KATIKA NJIA NIIENDEAYO NA KUNIPA CHAKULA NILE NA NGUO NI VAE NAMI NIKIRUDI KWA AMANI NYUMBANI KWA BABA YANGU NDIPO BWANA ATAKUWA MUNGU WANGU"
Kuna Mambo ambayo bila Shaka mimi nawewe tunaweza kujiuliza Kwa nini YAKOBO aseme maneno kama hayo ...kwani Mungu hakuwa wakwake hapo kwanza🤔🤔 ebu tuone hayaa👇🏻👇🏻
1: Licha ya kuwa natoka kwenye familia/ukoo Wa watu wenye agano na Mungu lakini mimi Binafsi naonaa ulazima Wa kuwa na Mungu wangu
2: Hata kama Mungu alikuwa akitulinda nilipokuwa Kwa wazazi wangu ni Kwa sababu ya Agano walilofanya wao ...Mimi namhitaji awe Mungu wangu
3: Ijapokuwa Mungu anaweza kunijibu Maombi yangu nikiwa Kwa wazazi wangu lakini upo umuhimu Wa Mimi kumtafuta Mungu wangu
4: Mungu anaweza kuwa upande wangu hata kama amefanya agano na baba zangu
Yakobo alichokuwa anakitafta ni kutengeneza uhusiano wake Binafsi na Mungu na kutafta Mungu awe upande wake
👉🏻 Wapo watu wengi ambao wamezaliwa kwenye nyumba/familia za waliookoka lakini hata siku moja hajawai kuchukua hatua ya kumtafuta Mungu Wa kwao Binafsi......
📥📥Chukua hii itakusaidia ...
Hata kama Mungu anakujibu ukiwa ndani ya familia iliyookoka ni lazima utoke ukamtafte Mungu Wa kwako ...Tengeneza uhusiano wako Binafsi na Mungu
📌 Kuzaliwa kwenye familia/Ukoo unaomfahamu Mungu hakumfanyi Mungu awe upande wako mpaka utakapo amua kumtafuta Mungu Wa kwako mwenyewe.....
📌UHUSIANO alioutengeneza Yakobo (Israel)na Mungu wake ulimfanya Mungu kumlinda miaka 20 aliyokaa kwa Laabani mjomba wake
📌Nini nimejifunza hapa Kwa Yakobo kwenye eneo la UHUSIANO WAKE NA MUNGU....
Kuwa na uhusiano Binafsi na Mungu utakusaidia Kwa sehemu kubwa na hichi ndicho Yesu alikuwa akikifanya Mara nyingi baada ya kumaliza kuhubiri mchana usiku alienda kutengeneza uhusiano wake na Mungu Kwa Maombi....
Maombi ya kikundi chako cha maombi hayamfanyi Mungu kuwa upande wako Ila upande Wa kikundi chako hivyo MTAFUTE MUNGU WAKO NA TENGENEZA UHUSIANO WAKO BINAFSI NA MUNGU.....
@Dennis Mushi 
#KingdomRepresentative
Previous
Next Post »