JIFUNZE KWA YAKOBO_Sehemu ya Pili

Na Denis Mushi
Moja kati ya vitu ambavyo nimekuwa nikivitafakari Kwa upana juu ya YAKOBO ni eneo hili la Mahusiano (relationship) simaanishi uhusiano wake na Mungu hapa nazungumzia ule uhusiano mwingine tunaoufahamu
Biblia inasema YAKOBO alisota miaka 14 Kwa ajili ya Rahel aliempenda Sana lakini haikuwa mpango Sanaa Kwa YAKOBO kukaa miaka yote hiyo Ila ni kutokana na desturi na mazingira pia aliyokuwa Kwa wakati ule yalimuamulia kusubiri Kwa miaka 14.
Ebu tusome MWANZO 29:18
"Yakobo akampenda Rahel akasema nitakutumikia Kwa miaka Saba Kwa kumpata Rahel binti yako mdogo"
Yakobo kama walivyo vijana wengine wakiume alikuwa akitamani kuwa na Mpenzi...na Biblia imeweka wazi kabisa kuwa Yakobo aliempenda Rahel...
Kwenye tafsiri ya kingereza anaelezea vizuri
"And Jacob loved Rachel because she was BEAUTIFUL and ATTRACTIVE"
Kila kijana Wa kiume anapenda kuwa na mschana mzuri tena anayevutia ...
Yaani mwenye figure..πŸ˜‚πŸ˜‚
Wengine wanasema awe portable πŸ˜‚πŸ˜‚na vijisifa vingi tunavijua sisi vijana Wa kiume....
Ndivyo ilivyo kuwa Kwa Yakobo ijapokuwa Biblia haijaeleza vyote hivyo ...
Yakobo aliempenda Rahel na aliamua KULIPA GHARAMA ya kutumika miaka Saba ili ampate Rahel.
Kitu cha ajabu kinachonifanya nijifunze hapa Kwa Yakobo ni Kuwa
Jacob served seven years for Rachel and they seemed to him but a few days because of LOVE he had for her....
πŸ˜‚πŸ˜‚ Kweli Yakobo umenipa changamoto hapa yaani kuona siku 2562 (miaka Saba) Kuwa siku chache na huku kata tamaa ukapambana .... kweli wewe ni kijana Wa kuigwaa😊😊
Kuna vitu nimejifunza hapa ngoja nikupatieπŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»
πŸ“ŒKabla Yakobo hajaanza kuingia kwenye mahusiano na Rahel alihakikisha anatengeneza kwanza uhusiano wake na Mungu
πŸ“ŒHaikumpa shida Yakobo kuisotea miaka Saba sababu ya Upendo aliokuwa nao juu ya Rahel...sasa wewe kukaa mwaka tu huwezi...
πŸ“ŒYakobo hakuwahi kukata tamaa wala kufanya jambo lolote nje na makubaliano katika kipindi chote cha miaka Saba...
πŸ“Œ Uvumilivu aliokuwa nao Yakobo ulimfanya kuiona miaka Saba Kuwa ni siku chache kwake Kwa sababu sifa moja wapo ya Upendo ni kuwa na tabia KUVUMILIA
πŸ“Œ Licha ya Yakobo kushindwa kumpata Rahel Kwa hiyo miaka Saba bado alikubali kuitumikia miaka mwingine Saba ili ampate Rahel....
MAMBO SITA AMBAYO ROHO MTAKATIFU AMENIFUNZA NA NINA IMANI YATAKUSAIDIA NA WEWEπŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»
Jambo la kwanza
πŸ“ŒKamwe usijaribu kujiingiza kwenye mahusiano kama hujaweka uhusiano wako na Mungu vizuri
Jambo la pili..
πŸ“ŒUsiwe na haraka ya kuingia kwenye mahusiano kabla miaka yako saba ya kushughulika haijaisha ... biblia inasema "Yeye aaminiye hatafanya haraka"
Jambo la tatu
πŸ“ŒKuwa na uvumilivu unapoingia kwenye eneo la Mahusiano...usikurupuke ...
Jambo la nne
πŸ“ŒAdui anaweza kukubadilishia Rahel wako japo umesota miaka saba.. Maombi ni ya muhimu sana πŸ™πŸΌ
Jambo la tano
πŸ“ŒUsiwe na haraka kumjua Raheli unapoletewa uwe mwangalifu sana usijekuta ni Lea ameletwa .
Jambo la sita
πŸ“Œ Mungu atahakikisha anamlinda Raheli wako hata kama uta sota miaka kumi na nne...
KUMBUKAA HILI ...
Uhusiano wako na Mungu ni jambo la msingi la kutengeneza kabla hujawa na uhusiano na mtu mwingine.....
Previous
Next Post »