PACKAGE OF TODAY: Usikimbie kuchakatwa

 

Zipo nyakati Mungu huruhusu tuzipitie ili kututengenezea tabia. Tusingejua kuvumilia kama tusingepita mahali pasipovumilika tukavumilia, Tusingejua kupenda kama tusingepita mahali penye chuki lakini tukadumu kupenda. Tusingejua kusamehe ni nini kama tusingekutana na matukio yaliyo magumu kusamehe lakini tukasamehe. Kupenda hakudhihirishwi kwa kuwepo kwa vinavyopendeka, ila visivyopendeka, wala kuvumilia kwa vinavyovyumilika, ila visivyovyumilika, pia kusamehe kwa vinavyosameheka ila visivyosameheka. Usikimbie kuchakatwa, Unatengenezewa tabia🥰

https://t.me/packag4

Previous
Next Post »