Njiti ya kiberiti ni ndogo sana na imetengenezwa na vijiti vidogo vidogo, tena garama ya kiberiti kwa nchi yetu huanzia shilingi mia, lakini Njiti hiyo ndogo ya kiberiti inaweza kuunguza msitu mkubwa sana na kuleta hasara kubwa mno inayozidi garama ya kiberiti..
Katika maisha Kuna kitu ambacho kikitumika sawa sawa kinaweza kuleta matokeo makubwa yanayozidi garama ya hicho kitu..
Leo nataman uone umuhimu wa wazo, idea, ndoto... Wazo/idea ni kitu kidogo sana lakini ukitumia wazo au idea unayoipata katika Akili yako inaweza kukuleta matokeo makubwa kuliko hata garama uliyoitumia kuwaza hicho kitu.. Wazo ni kitu cha thamani zaidi ya Pesa.. Unaweza kuwa na pesa nyingi lakini kama huna mawazo ni sawa na kuwa na gari Bila mafuta..
Mara nyingi Mungu hutumia mawazo yetu kupitisha Ile taswira ya jinsi anavyotaka tuishi.. Lakini mara nyingi tumekuwa watu wa kupuuzia juu ya idea au mawazo yanayokuja ndani yetu..
Ni kweli unandoto za kuwa muimbaji mkubwa, mwana siasa, mwalimu, muhubiri n. K lakini ni kwa jinsi Gani umekiwa ukiishi kwa kufata Wazo ulilonalo akilini..?
Ngoja nikukumbushe... Waimbaji wengi wakubwa au wahubiri wakubwa unaowaona au waandishi wa vitabu wote walianzia kwenye kitu kinachoitwa idea.. /wazo.. Hakuna mtu alikurupuka Bila kuwaza kwanza.. Hata Mungu alipotuumba sisi hakuanza tu kuumba Ila alianza kwa mfumo wa idea/wazo.. Thus why akawa anasema na tumfanye mtu kwa sura yetu... Lakini ukiendelea mbele utakuta biblia inasema ndipo Mungu akachukua udongo akamuumba mwanadamu.. Sasa katika kila kitu tunachofanya kinaanzia kwenye idea .. Kujenga nyumba kunaanzia kwenye idea /wazo.. Hata unapoenda kushona nguo ni lazima uwaze kwanza ndipo uchukue hatua ya kwenda kwa fundi .
Hata katika suala La kuoa au kuolewa mara nyingi huanzia katika idea.. Na badae kudhihirika katika ulimwengu wa kimwili.. Yani unaweza kuimagine juu ya familia yako itakavyokuwa hata kama hujaoa au kuolewa.. Yote haya nataka kukuonesha ninini umuhimu wa idea /wazo..
Epuka sana kukana wazo au idea nzuri inayokuja kwenye ufahamu wako ambayo unahisi itakuletea matokeo chanya...
📌tupo duniani tunaishi katika ulimwengu wa kimwili ambao chanzo chake ni ulimwengu wa Roho.. Sababu tunajua vyote vinavyoonekana vimetokana na visivyoonekana.. Na ndio maana dhana kubwa aliyetumia Mungu katika kuumba (kuvileta vile visivyoonekana kwenye vinavyoonekana) ilikua ni Neno... Mungu alikuwa anasema naiwe Anga , jua etc na vilikua vinatokea..
📌Mawazo au ndoto ulizonazo ni muhimu sana.. Idea uliyonayo hata kama ni ndogo inamatokeo makubwa sana katika maisha yako.. Matokeo hayo yanaweza kuwa chanya au hasi (positive au negative)
Itaendeleaaaa
Facebook | | Instagram | YouTube
Email: judithmbilinyi@gmail.com
Tel: +255 762 372 408
Maoni yako hapa
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon