Hii ilikuwa ni baada ya kuhitimu masomo yake katika chuo cha Mwenge ambako alipata Shahada ya Ualimu. Baada ya kuona watu wanaoteseka na kuonewa na shetani, wanaokata tamaa na kuvunjika moyo, watu wasioamini kwamba Mungu yupo na anayeweza kuokoa, kiu yake kubwa ni shauku yake ni kuwafikishia watu habari njema za Yesu Kristo kwa njia ya uimbaji. Anatamani kumwambia kila mtu kwamba Mungu yupo. Akiongea na Sound Of Worship anasema "I need to tell every body in this world who God is", kwamba nataka kumwambia kila mtu Mungu ni nani. Anaomba Mungu amwezeshe aweze kuwafikia watu wake katika huduma hii na Roho Mtakatifu awajaze wote watakao sikia.
Kazi ya pili kutoka kwake Fadhili Efron inategemewa kutoka mwezi wa pili. Kazi hii ni wimbo MUNGU UNATAWALA, ambayo ni 'Hip Hop Gospel' akiwa amemshirikisha mwimbaji Novic.
Changamoto anazokutana nazo ni kukosa muda wa kuandaa nyimbo kwani anakuwa amebanwa na majukumu mengine ya kijamii. Pamoja na changamoto hii, Fadhili haachi kumwambia Mungu amtumie vile apendavyo ili afikishe habari njema kwa wale waliokusudiwa. Pia amsaidie apate watu wa kumuunga mkono katika kuifanya kazi hii kwa michango yao ya maombi, mawazo na fedha.
Mawasiliano:
Facebook | YouTube |
WhatsApp/Simu: +255 766 004 196
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon