Maisha ya kiroho II


Maisha ya kiroho ni mapana na hayaeleweki kwa akili, maana maisha haya yapo ndani ya ulimwengu usioonekana kwa macho ya damu na nyama, yaani ulimwengu wa Kiroho.

Katika ulimwengu huu, Roho ya Mungu inatawala na kutenda kazi pamoja na watakatifu walioko hai duniani.
Lakini pia katika ulimwengu huo wa roho, roho ya giza ipo ikifanya upinzani na kwenda kinyume na kila agizo litokalo kwa Baba dhidi ya watakatifu waisikilizao sauti ya Mungu. Roho hii ya giza inatawala na ina wafuasi wake ambao wapo na binadamu hai pia...
Katika maisha ya rohoni, Mungu anampa nafasi mwanadamu hai kuwa na "access" katika ulimwengu wa roho kwa njia ya Imani.
_Hivyo mtu huyu ataweza kuona, kusikia, kutenda katika namna isiyoeleweka na akili ila Imani pekee._
.
.
MAISHA ALIYOKUSUDIA MUNGU
Kuishi maisha ya rohoni ndio nafasi ambayo Mungu alimpa mtoto wake aishi... ili aweze kuwa na ufanisi katika kutenda, kusikiliza, kuona sawasawa na mapenzi yake Mungu mwenyewe kwa njia ya kuzaliwa mara ya pili.
Kumbuka:
Yohana 3:3
Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.
Jiulize maswali haya kuongeza tafakari:
Ufalme wa Mungu uko wapi?
Je, naweza kuishi ndani ya ufalme sasa?
Je, ninawezaje?
Turudi hapa:
lli kuwe na maisha ni lazima kuwe na
uhai.
"Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; *mtu akawa nafsi hai.*"
Mwanzo 2:7
*Ndani ya maisha* kuna shughuli mbalimbali ambazo zinamuhitaji *mtu hai* akiwa mwenye afya na uelewa aweze kufanya au kuenenda nazo.
"Bwana Mungu _akamtwaa huyo mtu,_ *akamweka* katika bustani ya Edeni,
*ailime na kuitunza.*"
Mwanzo 2:15
_Kwakuwa mtu hai anahitaji kukuta mazingira ya kumfanya aishi, Mungu aliandaa hayo mazingira._
"Bwana Mungu *akapanda bustani* upande wa mashariki wa Edeni,
*akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya.*"
Mwanzo 2:8
Kwakuwa mazingira yalikuwa na uhitaji wake, Mungu alijua namna sahihi ya kukidhi kile alíchokiona
kinahitajika kifanyike kwa hayo mazingira.. *(Yaani siri ya hitaji la kimazingira, mahala Mungu anahitaji uwepo lipo ndani ya Mungu mwenyewe aliyeandaa mazingira.)*
KUMBUKA:
- Somo ni maisha ya kiroho.
- Mungu ni Roho.
- Mungu anatenda kazi zake kupitia watakatifu wake waliopo duniani, waishio kwa namna ya mwili.
- Mungu anamuhitaji mtakatifu huyu awe mahala ambapo *"Network yake na Mungu"* zitakamata sawasawa. ROHONI.
TUENDELEE:
"Hapakuwa na mimea juu ya nchi wala miti haikuwa imechipua kwani Mwenyezi-Mungu hakuwa ameinyeshea nchi mvua, *wala hapakuwa na mtu wa kuilima."*
Mwanzo 2:5
*Jambo lolote linalofanywa na mtu hai kumfanya aendelee kuwa hai limeratibiwa katika roho.*
Na ufalme upi, wa giza au wa nuru hilo ni jambo la kimahusiano au nguvu ya mtu huyo dhidi ya hizo falme.
Kwa lugha nyepesi;
_Ulimwengu wa mwili ni udhihirisho wa mambo yanayoendelea katika roho._
"Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, *ailime na kuitunza.*
Mwanzo 2:15
Nahitaji uone mahusiano ya Ulimwengu wa roho na maisha ya kawaida.
*Si kwamba maisha ya kawaida ya mwilini ndio yataamua maisha ya rohoni... bali maisha ya rohoni ndio huamua hatma ya maisha yako ya mwilini sasa.*
Usipoelewa rohoni unatakiwa kufanya nini eneo ulilopo sasa,... basi ni rahisi kutumikia falme usiyoijua.
Hatuishi kwa bahati mbaya, ila kuna mpango maalum kwa kila aliyefanyika kiumbe kipya... na mpango huo ni kutimiza mapenzi ya Baba.
Tunayajuaje mapenzi ya Baba? Ni kwa njia ya Roho mtakatifu.
*Yohana 16:13*
Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; *kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.*
Previous
Next Post »