Maisha ya kiroho III


 UHUSIANO WA KIMAZINGIRA NA MAISHA YA KIROHO _(Kwa waliokubali kuongozwa na Roho mtakatifu)_

"Hapakuwa na mimea juu ya nchi wala miti haikuwa imechipua_ kwani Mwenyezi-Mungu hakuwa ameinyeshea nchi mvua, wala hapakuwa na mtu wa kuilima."
Mwanzo 2:5
"Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza.
Mwanzo 2:15
Mtu hai aliandaliwa mazingira, ili aweze kuenenda nayo kwa kadiri ya uhitaji wa mazingira hayo, (sawa sawa na mapenzi ya Mungu)
Hivyo mtu hai (aongozwaye na Roho) hana uwezo wa kujiandalia mazingira yaliyo sahihi, ila Mungu pekee. Kwa sababu, kusudi la pale ulipo, lipo ndani ya yule aliyekuweka. Anajua uwezo wako na hitaji lako kulingana na mazingira aliyokuweka, pia anajua
namna ya kukufanya uishi.
Je, upo hai?
Je, upo katika mazingira ambayo Bwana anahitaji uwepo?
Je, unalohangaikia sasa ni sehemu ya lile Neno la Bwana "Ailime na Kuitunza?" (yaani unalotenda au kuliishi linatokana na mpango wa Mungu) _au unahangaikia kujishonea majani na kutafuta pa kujificha mbali na uso wa Bwana?
Mazingira yana support uhai wa viumbe vyote, kama ilivyokuwa Eden.
Lakini Mungu alidhamiria Uhai wetu (Roho zetu) ushikiliwe na Taswira ya mazingira iliyopo moyoni mwake (Mungu) kwanza ndio ije nje kwenye uhalisia.
Hivyo Bwana aliujaribu ufahamu wa Adam aone analoliwaza kwenye yale mazingira ni kile kilichomo ndani ya moyo wa Baba ake? (Yaani Mungu).
*Mwanzo 2:19*
Bwana Mungu akafanyiza kutoka katika ardhi kila mnyama wa msituni, na kila ndege wa angani, *akamletea Adamu _ili aone_ atawaitaje;* kila kiumbe hai, jina alilokiita Adamu likawa ndilo jina lake.
"Ili aone..."
The Lord God took soil from the ground and he made all the animals and birds. Then he brought them to the man. *_God wanted to know_ what names the man would call them.* Whatever the man called each living thing, that became its name.
Genesis 2:19
Adam aliwaza sawasawa na yaliyo moyoni mwa Baba. Muunganiko wao ulikua perfect.
Adam aliishi katika mwili lakini alimiliki menu ya maisha kutoka kwa Baba. Adamu alikua na access kamili na Baba.
.
.
Shetani alitambua tangu awali kuwa, mtu hai hana maisha sahihi nje ya maelekezo ya yule aliyemuweka katika
bustani _"ili ailime na kuitunza"_ Ndipo
akaleta maelekezo yake mapya.
Hakuna maisha nje ya maelekezo ya Mungu. *Mpango wa Mungu ni kutufanya tuone mipango na mikakati yake juu yetu kwa mtazamo wake (wa rohoni - kama alivyokusudia)* na sio kwa mtazamo wa mwilini.
Maisha aliyotamani kuyaona Shetani kwa mtu hai (Mwanadamu) ni yale ya
kujihangaikia mbali na msaada wa Mungu.
Yaani mtu hai aone maisha na mazingira yake kwa namna ya mwilini.
*Ubora wa maisha upo mahali ambapo Mungu amehitaji uwepo.*
_Ndani ya maisha aliyokusudia Mungu ndipo ufalme wake ulipo._
_Huwezi kuuona ufalme wa Mungu kama haupo ndani ya ufalme huo._
.
.
*B. UHUSIANO WA KIMAZINGIRA NA MAISHA YA KIROHO* - _(Dhambi ilipopata nafasi)_
*Dhambi* ina tabia ya kufisha au kuua.
Kwanza inaua ufahamu wa mtu hai kwa kuifisha ile taswira ya mazingira iliyopo moyoni mwa Baba kwako.
_(Yaani inaua macho ya rohoni, inafisha mitizamo ya KiMungu)_
*Mwanzo 3:7* *Wakafumbuliwa macho* wote wawili *wakajijua* kuwa wa uchi, *wakashona* majani ya mtini, wakajifanyia nguo.
Dhambi ilipopata nafasi kwa Adam na Hawa, punde...
1. Wakafumbuliwa macho
Adui akaua macho yaliyoona sawasawa na mapenzi ya Mungu.
Hapa ndio eneo ambalo watu wengi tunaingia kukatia tamaa mambo mazuri tuliyopanga kuyafanya kabla dhambi haijapata nafasi.
Tafakari:
Unawaza kufungua biashara ya Chips, Mungu anahuisha wazo lako unapata nguvu ya kulifanyia kazi... Ghafla; Dhambi inakupitia... bila kuwa aware imekuja ilikua ina winda nini, unaanguka dhambini...
Rafiki yangu lile wazo haliwezi kubaki kama lilivyokuwa... utakata tamaa na hautaiona ile nguvu ya awali, na badala yake kila neno la kuponda biashara ya chips ukilisikia utaliona ni kweli.
(Mambo haya nimeyashuhudia kwenye tafiti za maombezi ya deliverance na ushauri)
Ukiona hivi ujue kabisa
2. Wakajijua (umejijua) wako Uchi
Kwamba wazo lako lilikua linakupoteza, halikua sahihi... ungepata hasara, ungeaibika, watu wangekucheka...
Then, unaamua
3. Kushona majani ya mtini
Unajitafutia kazi ambayo unahisi kwa akili zako ndio inafaa zaidi...
_tambua haya ni mawazo ya uharibifu, maana yanaondoa maana ya kuitunza bustani na kuilima na kuingia kukata majani na kuyapa matumizi yasiyo sahihi._
Kuamua kufanyia kazi mambo yako nje ya agizo la Mungu ndio mwanzo wa anguko lako.
Macho ya rohoni hayamuoni Mungu tena,..
Macho ya mwilini yanakutazamisha aibu uliyonayo, utakayoipata...
Kuna watu wanaishi sasa na wanaamini UONGO wa hii aibu aliyoiona ADAM ndio Ukweli wa maisha.
SI KWELI.
Ukweli ni upi? Baba anataka tuone jambo hili leo... kama tunahitaji kufumbuliwa macho yale ya awali sawasawa...
*Mathayo 6:25*
Kwa sababu hiyo _nawaambieni,_ *Msisumbukie maisha yenu,* mle nini au mnywe nini; *wala miili yenu,* mvae nini. *Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?*
*Mathayo 6:26*
Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na _Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao._ Ninyi je! Si bora kupita hao?
*Mathayo 6:27*
Ni yupi kwenu ambaye *akijisumbua* aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja?
*Mathayo 6:28*
*Na mavazi, ya nini kuyasumbukia?* Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti
*Mathayo 6:29*
nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo.
*Mathayo 6:30*
Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, *enyi wa imani haba?*
*Mathayo 6:31*
*Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?*
*Mathayo 6:32*
Kwa maana *hayo yote Mataifa huyatafuta;* _kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote._
*Mathayo 6:33*
*Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.*
Previous
Next Post »