Maisha ya Kiroho IV

 


C: KWELI NI MSINGI WA MAISHA YA KIROHO.

Kweli (Truth):
1. Kweli ni taarifa sahihi,...
2. Kweli ni Neno la Mungu.
3. Kweli ni Mungu.
UONGO:
Uongo ni yale yote yanayopingana na Kweli.
▪︎Uhusiano wa "Kweli" na maisha ya kiroho.
Yohana 1:1
Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
Yohana 1:3
Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.
Yohana 1:4
Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.
Kwakuwa Mungu ndio Kweli, nayeye ndie Neno, na kwa njia ya Neno vitu vyote vilifanyika, basi Mungu ndie asili ya vitu vyote.
Ndani yake Neno (Kweli) ndimo ulimokua uzima.
Tujiulize mpaka hapo, mtoto wa Mungu anaweza kufanikiwa katika mwili kama hajafanikiwa katika roho?
Walio wa ulimwengu wa giza pia hutafuta mafanikio katika roho kwanza.
Hivyo ni dhahiri, siri ya maisha halisi imefungwa katika maisha ya rohoni.
Kwa maana asili ya maisha halisi imeanzia rohoni.
Asili ya uhai imeanzia rohoni, pumzi ya Baba.
Tujiulize swali; kama uzima wa yule Neno, ambae ndie kweli,... ndio ulikua nuru ya watu,.. Je, maisha ya mtoto wa Mungu yanaweza kuwa na nuru nje ya hii Kweli?
Nahitaji uone kwa namna gani maisha yako halisi yalivyofungamanishwa na maisha yako ya rohoni.
Matokeo ya unavyoishi sasa yalianzia rohoni... tazama hili kwa mapana.
*Yohana 1:5*
*Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza.*
Kweli ikiongoza maisha yako, hakuna uongo utakuweza.
Ukiishi maisha ya Kweli (maisha ya kuongozwa na Roho mtakatifu) *uongo unakukataa.*
Kweli pekee ndio hutuweka huru.
*Yohana 8:31*
Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi *waliomwamini*, Ninyi *mkikaa katika neno langu,* mmekuwa wanafunzi wangu _kweli kweli;_
*Yohana 8:32*
tena *mtaifahamu kweli,* nayo hiyo kweli *itawaweka huru.*
*Neno la Mungu ni UHAI usioweza kuuona kwa macho ya nyama...*
_Na wala huwezi kulielewa kwa akili za kawaida._
Kwasababu NENO ni MUNGU.
***
Adui au ufalme wa giza hupambana sana na *ufahamu wa mtoto wa Mungu.*
Huanza kutafuta huyu mtoto wa Mungu anajua nini? Huwa anaona nini? Huwa anasikiliza kwa kiwango gani? *Adui hupima una Ukweli kiasi gani moyoni?*
Pitia mazungumzo ya nyoka na Hawa, tazama alichojibu Hawa... "wala msiyaguse"... hili neno Mungu alipoongea na Adam halikuwepo au halikutumika.
Kutokuwa na taarifa sahihi (NENO SAHIHI) ni nafasi ya adui kupita...
.
.
*JIULIZE:*
Ni maeneo gani yanahitaji kufunguka katika maisha yako.
Ukiweza kujiuliza swali hili, liboreshe kwa upya; ni maeneo gani unahitaji kumsikia Mungu waziwazi akikueleza ufanye nini.
Kama umejiuliza vizuri hili swali, liboreshe zaidi; *ni maeneo gani kwenye maisha yako yanahitaji UKWELI?*
Maisha bila Kweli hakuna maisha.
Uongo una sumu ya mauti.
Inafisha kila kitu...
yaani naomba uelewe hapa nikisema inafisha *maana yake vinakosa access ya kuhuishwa kwa njia ya maombi.*
*Huwezi kuuombea uongo uwe ukweli. Ila unaweza kuuacha uongo na kuuchagua ukweli.*
Je, unafikiri ni jambo rahisi kuuacha uongo? (Maneno yote yaletayo upinzani na Neno hai la Mungu) Neema ya Mungu pekee hutusaidia hapa.
Yesu ndie _Njia,_ na *Kweli na Uzima.*
Shetani ni muongo na baba wa huo. *Hajawahi kusema kweli na wala hiyo kweli haimo ndani yake.*
Ukweli ni uponyaji ndio maana tunawekwa Huru kupitia huo.
Maisha ya kweli hutuweka mbali na dhambi...
Napozungumza kuhusu Ukweli na Uongo sihitaji uone eneo la kuzungumza ukweli au kuzungumza uongo.
Natamani uuone mfumo wa Kimaisha ambao mwanadamu akiuchagua anaweza kuuona uzima au mauti.
Ukweli huu ni yale ambayo mtoto wa Mungu ameyakubali na hana shaka nayo moyoni mwake...
Ukweli huu ni yale ambayo ameamua kuyaishi hata kama atapitia changamoto gani
Ukweli huu umeanzia ndani yake na unadhihirika mpaka nje...
Mtu asiye na hila.
Maana mwenye hila hubeba jambo lenye sura ya kweli na kulitegesha mahali ili limkwae mwingine, kisha mtu huyo apate kutimiza jambo lake alilokusudia... huo ni UONGO... ni kama ibilisi atumiavyo Neno la Mungu ili kuwaingiza kwenye mtego walio dhaifu.
.
.
Kwahiyo Ukweli au Uongo ni tabia hai zinazoweza kukujengea au kukuharibia mipango yako kuanzia rohoni kuja mwilini.
Kwa sababu Utakatifu ni matokeo ya kuufanyia kazi ukweli na Dhambi ni matokeo ya kuufanyia kazi uongo.
*Mathayo 5:37*
*Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.*
Mungu anakuhitaji uishi maisha ya Kweli. Yaani kile ulichonacho rohoni mwako lile ulijualo ndani yako, lile ambalo umelikiri na kuliamini kwa Bwana lionekane mpaka nje.
Yaani nikisema Hapana sina, kusiwe na hila au neno lolote linalonidai ndani.
Maisha yangu yawe wazi mbele za Baba. Nina njaa? Nina furaha? Nina huzuni? Nina shukurani? Ni hitaji? Haya yote na yajulikane mbele za Baba.
*Wafilipi 4:6*
Msijisumbue kwa *neno* lolote; *bali katika kila neno kwa kusali na kuomba,* pamoja na kushukuru, *haja zenu na zijulikane na Mungu.*
*Wafilipi 4:7*
Na amani ya Mungu, *ipitayo akili zote,* itawahifadhi mioyo yenu *na nia zenu* katika Kristo Yesu.
*Namba ya kuufundisha moyo kusimama kwenye kweli.*
*Wafilipi 4:8*
Hatimaye, ndugu zangu, *mambo yoyote yaliyo ya kweli,* yoyote yaliyo ya staha, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote yenye kupendeza, yoyote yenye sifa njema; ukiwapo wema wowote, ikiwapo sifa nzuri yoyote, yatafakarini hayo.
Mambo ya Mungu yamekua ni magumu sana kwasababu mwanadamu aliamua kuuamini uongo na kuukubali.
Hatuteswi na Ukweli bali tunateswa na uongo tulioukubali. Ndio maana shetani kila siku anapanda uongo ili maisha ya kiroho yawe magumu zaidi.
Ukweli unaweka huru.
Mfano:
Uongo unaweza kusema Kilimo ni kazi mbaya na ngumu ambayo Mungu hawezi kunichagulia.
Ukweli unasema Adam aliwekwa bustanini alime na kutunza hiyo bustani. Na ndio eneo adam alikua huru.
Kwahiyo inawezekana mateso unayopitia sasa kuna uongo ulioukubali nyuma yake... na uongo huo utaleta mauti (vitu havitasimama au zaidi ya hapo) kama hautofanyiwa kazi sawasawa.
Lakini unaweza pia kuukubali ukweli na ukapitia mateso lakini Bwana akakuhifadhi na ukweli huo ukaleta Uzima.
Kama Kristo..
*Zaburi 34:19*
Mateso ya mwenye haki ni mengi, *Lakini Bwana humponya nayo yote.*
*Zaburi 34:20*
Huihifadhi mifupa yake yote, *Haukuvunjika hata mmoja.*
*Ukiwa na Kweli ya Mungu, maisha yako yatajaa Kweli. Ukiwa na uzima maisha yako mpaka vitu vyako vyoote vitatokana na Uzima huo, navyo vitabeba Uzima,... halleluia.*
Taz.
1. Ayubu na mali zake
2. Yesu na Kanzu yake
3. Paulo pia
*Matendo ya Mitume 19:11*
Mungu akafanya kwa mikono ya Paulo miujiza ya kupita kawaida;
*Matendo ya Mitume 19:12*
hata wagonjwa wakaletewa *leso na nguo zilizotoka mwilini mwake, magonjwa yao yakawaondokea, pepo wachafu wakawatoka.*
Previous
Next Post »