Maisha ya kiroho V


 NAFASI YA IMANI KATIKA MAISHA YA KIROHO

Waebrania 11:1
Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
Kutokana una ufafanuzi huu wa Biblia kuhusu imani basi ni wazi mwenye imani anapata access moja kwa moja ya rohoni.
Maisha ya Kiroho hayawezekani bila Imani. Hakuna mawasiliano bila BANDO.
Hatuwezi kumuona Baba bila Imani. Hatuwezi kumpendeza na kujua yampendezayo bila imani.
Hatuwezi kuyafuata mambo ya rohoni bila imani.
Waebrania 11:6
Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; _kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko,_ na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.
Neno la Mungu linatueleza vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri...
Waebrania 11:3
Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri.
Hii inatuonesha wazi ili mtoto wa Mungu afanikiwe katika mwili ni lazima afanikiwe kwanza katika roho.
Kwanini?
Kwa sababu mafanikio yatokayo katika roho hudumu na huwa na kibali, huwa na chapa ya Kristo maana yametokana nae. Na Mungu atatukuzwa kwa mafanikio hayo.
***
Imani huuona ukweli.
Imani huufunua ukweli.
Imani ndio kiunganisho kati ya ulimwengu wa roho na mwilini.
Hofu ni imani ya kuzimu, kwasababu inakuonesha UONGO na kukuficha UKWELI.
Hofu haioni nuru bali giza. Katika hofu hakuna uhakika bali kujaribu na kubahatisha.
Hofu ina adhabu na mahangaiko.
_Kwa kifupi sana Hofu ndio chanzo cha maswali yasiyo na majibu, Bali imani huweka bayana mambo yote._
*Yakobo 1:5*
Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.
*Yakobo 1:6*
Ila na aombe *kwa imani,* pasipo *shaka yoyote;* maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.
*Yakobo 1:7*
_Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana._
*Maisha ya Kiroho yanaongozwa na Imani, ili itusaidie kuielewa ile Kweli ya Neno itokayo katika Roho.*
.
.
*NAWEZAJE KUISHI MAISHA YA KIROHO WAKATI NIPO KATIKA MWILI?*
Wanaoweza kuishi maisha ya Kiroho (yaliyo sawasawa na mapenzi ya Mungu) ni wale waliofanya maamuzi ya Kumsikiliza na kumfuata Roho mtakatifu.
*Warumi 8:14*
Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, *hao ndio wana wa Mungu.*
*Mwanadamu mwenye nguvu ni yule mwenye access katika roho ya kumiliki na kutawala.*
Sasa kuwa katika mwili its not an excuse maana hata wachawi na waganga wanaishi katika roho kwa kusikiliza mambo yao ya giza.
Lakini pia kwa mtoto wa Mungu kuishi katika mwili umefanya kukosa masikio na macho ya kukuwezesha kuona na kusikia kutoka kwa Baba (rohoni) kwahiyo utalitumikia kusudi la shetani tuu maana lisilotoka kwa Mungu hutoka kwa Muovu.
Mtoto wa Mungu akiishi katika roho anakua mbali na dhambi...
Kwanini?
- Kwasababu anaona yote kwa njia ya imani
- Kwa njia ya imani hiyo huipokea neema ya Mungu.
- Hana hofu ndani yake.
- Kwakuwa hana hofu (kwakua hofu hutuonesha uongo) basi hana kujihukumu maana Kweli (Kristo) anaishi ndani yake.
*Warumi 8:1*
Sasa, basi, *hakuna hukumu ya adhabu* juu yao walio katika Kristo Yesu.
*Warumi 8:2*
*Kwa sababu* _sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru,_ *mbali na sheria ya dhambi na mauti.*
***
Sheria ya Roho wa uzima ule... ulio katika Kristo Yesu...
kumbuka Yesu ndie Neno na ndani yake ndimo ulimokua uzima, lakini ndie Kweli ituwekayo huru...
_Na kutuweka mbali na sheria ya dhambi na mauti_
Hatuwezi kuwa sawa katika maisha ya kiroho kama watoto wa Mungu... kama bado tuna hukumu iliyotushikilia katika mwili...
Ndio maana ili huyu mtoto wa Mungu apate full access katika roho bila hatia katika mwili akamtumwa mwanae Yesu (aliyekua katika roho) aje katika mwili *(eneo ambalo shetani ana access nalo pia... kwa maana sheria ya mwili shetani anapata kibali nayo na ndio anayowaibulia wanadamu hatia na kujihukumu)*
*Warumi 8:3*
Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, *Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili;*
Kwa uelewa zaidi tusome hapa:
The Law that God gave to Moses *could not make us free like that.* _We were too weak to obey his laws because we are human._
But God has done what his Law could not do. *He sent his own Son to become a person like us.* _His human body was like the body of people who do wrong things._ *God's Son died as a sacrifice to take away the punishment for our sins.*
In that way, _God destroyed the power of sin over people who are weak and human._
*Romans 8:3 EASY*
Kwanini Mungu alifanya haya kwa wanaotaka haya maisha ya rohoni?
*Warumi 8:4*
ili maagizo ya torati yatimizwe *ndani yetu sisi,* _tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili,_ *bali mambo ya roho.*
Kwa tafsiri zaidi:
God did this so that *we could become right with him.* _God's Law showed us how to be right with him._ *And now we can be right with God, if we live with God's Spirit as our guide.*
_We do not do what our weak human thoughts want us to do._
*Romans 8:4 EASY*
Kwa hiyo hili jambo alilolifanya Bwana Yesu ili kutupatia Full access katika roho bila kujihukumu, mbali na dhambi ndio NEEMA yenyewe kwa waishio katika ROHO katika ulimwengu wa roho.
Tulimsoma Adam kule mwanzo, aliporuhusu dhambi kuingia kwenye maisha yake,... mwili ulianza kumtawala na alianza kuwaza ya mwilini... akajishonea nguo,
lakini katika mwili hukumu huwa haibebeki na kujilaumu huja, Adam akaamua kujificha mbali na uso wa Mungu... maana uongo ulizaa hofu iliyomtazamisha Mungu hawezi kukuelewa tena wala hawezi kukusaidia...
Ndugu yangu alichokifanya Yesu ni ili tuweze tena kuishi katika roho kwa kufikiria kwa namna ya rohoni (yaani sawasawa na Baba kama alivyokua Adam kabla ya kuiruhusu dhambi) na tuweze kuona matokeo na mafanikio yenye chapa ya Kristo... maana kilichozaliwa kwa Roho ni roho.
Rejea:
*Yohana 3:6*
*Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.*
***
Mafanikio yatokanayo na maisha ya mwili (Nje ya Mungu) Hayadumu, hufa, hayana furaha, hayana utukufu, hutopata nafasi ya kupumzika, yatakutesa.
*Mafanikio yatokanayo na maisha ya rohoni (kuongozwa na Roho mtakatifu) Hudumu, huwa hai, yana furaha, humpa Mungu utukufu, utapumzika, hayatakutesa.*
.
.
*TAFAKARI ZAIDI YA MAANDIKO.*
*Warumi 8:5*
*Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho.*
*Warumi 8:6*
*Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani.*
*Warumi 8:7*
Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, *kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii.*
NB:
Haiwezi kutimiza mapenzi ya Mungu. Nia ya mwili ni kujitafutia mambo yake yenyewe | kujitetea | kujipambania... (kwasababu mwili huiona aibu mbele yake.)
*Warumi 8:8*
*Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu.*
NB:
Kwakua hakuna eneo utakutana nae, wala hakuna mahala utamuona. Hivyo kumpendeza pia sahau.
Mungu ni roho, watamfutao lazima waamue kuishi katika roho na si katika mwili. (Yaani kuongozwa na Roho mtakatifu).
*Warumi 8:9*
*Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho.* *_Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake._*
NB:
Mtoto wa Mungu,
Kuongozwa na Roho ili uishi maisha ya rohoni sio uchaguzi its not an option. Amua *sasa.*
*Warumi 8:10*
Na Kristo akiwa ndani yenu, _mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi;_ *bali roho yenu i hai, kwa sababu ya haki.*
*Warumi 8:11*
Lakini, ikiwa _Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu,_ *yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu.*
UNAWEZA UKASOMA HII WARUMI 8 YOTE KWA UTULIVU.
Lakini nimalizie hapa:
Ukiishi maisha ya Kiroho yaani kwa kuongozwa na Roho, utaweza kuisikia sauti ya Mungu waziwazi hivyo utaijua KWELI ya maisha yako na maisha yako yatakua na NURU ile nuru iletayo UZIMA na utapokea na kuona waziwazi kwa njia ya IMANI na haya yote yatakujia kwa sababu ya ile NEEMA iliyotuweka mbali na dhambi...
Basi kama katika roho tunakua na imani basi tunao ujasiri... ujasiri kutokana na yale tuliyoyaona na kusikia kwa njia ya imani...
*Warumi 8:38*
Kwa maana *nimekwisha kujua hakika* ya kwamba, _wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo,_
*Warumi 8:39*
_wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote_ *hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.*
Kwahiyo...
*Warumi 8:37*
*Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.*
Previous
Next Post »