Maisha ya kiroho VI


UHUSIANO WA UFAHAMU WAKO NA MAISHA YA KIROHO.

Ufahamu wako ni mzizi wa maisha yako ya Kiroho.
Kuna ufahamu (Understanding)
Kuna maarifa ( Knowledge)
Ufahamu ni uwezo wa kutafsiri taarifa, kunakopelekea kutambua maana au sababu ya kutokea, kufanyika au kuwepo kwa mambo mbalimbali.
Maarifa ni taarifa au utambuzi unaojengwa na uzoefu, elimu au mafunzo ya aina fulani.
Vinafanana kidogo lakini kuna tofauti ya matokeo...
Mfano:
Mwalimu anafundisha darasani wanafunzi wapate maarifa, lakini ufahamu baina ya mwanafunzi na mwanafunzi unatofautiana kulingana na uwezo wa mwanafunzi mmoja kuweza kutafsiri na kuelewa mafundisho yale kuliko mwingine.
That means they both can have Knowledge but they can differ in understanding.
Ufahamu ni muhimu sana kwasababu ndilo eneo linalopokea taarifa na kuzitafsiri,... katika mwili na zaidi katika roho.
Katika roho tunapokea taarifa kwa njia ya kusikia (masikio) kuona (macho) kuhisi na namna nyingine ambazo Mungu amekua akitumia kusema nasi.
Ili ufahamu wa rohoni uweze kufanya kazi sawasawa ni lazima roho iwe imepokea taarifa nyingi zaidi (maarifa) zilizo sahihi na za kweli kutoka katika ufalme wa Mungu.
Neno la Mungu ndio chanzo cha maarifa hayo naye Roho mtakatifu hutufundisha na kutusaidia kuyafahamu anayotuamuru Bwana.
Ufahamu wa rohoni hauongozwi na akili, kwa sababu akili hutuongoza kureason na kujudge, akili inahitaji vitu dhahiri ili vilete maana. Ufahamu wa rohoni huratibiwa na IMANI.
Warumi 10:17
Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.
Adui ili apate nafasi katika maisha ya mtoto wa Mungu huangalia udhaifu wake katika ufahamu dhidi ya Neno lile la kweli analodai kuliamini.
Mathayo 14:31
Mara Yesu akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka?
*Mathayo 15:28*
Ndipo Yesu akajibu, akamwambia, *Mama, imani yako ni kubwa;* na iwe kwako kama utakavyo. Akapona binti yake tangu saa ile.
*Mathayo 16:8*
Naye Yesu akafahamu, akawaambia, *Mbona mnabishana ninyi kwa ninyi, enyi wa imani chache,* kwa sababu hamna mikate?
Mwenye Imani haba ana taarifa sahihi chache, au ana taarifa lakini ana mashaka nazo.
*Nahitaji uone nguvu ya taarifa sahihi (Neno) katika ufahamu wako zinavyoweza kukusaidia kuishi maisha ya rohoni.*
Imani inatofautiana na akili kwasababu Imani imebeba taarifa zenye uhakika bila kutegemea ushahidi uliodhibitika katika mwili.
*Akili hupitisha mambo yaliyotafsiriwa na ufahamu kwa namna ya mwili, lakini Imani hupitisha mambo yaliyotafsiriwa na ufahamu kwa namna ya rohoni.*
Elewa jambo hili;
Kila neno ulitamkalo ni mawazo uliyoyakubali na kuyapitisha katika akili yako.
Mfano:
Mlevi ni ngumu kutawala mawazo au fikra zake kwasababu kilevi hufunika uwezo wa akili kuratibu matendo ya ufahamu.
Hivyo mlevi au chizi hawezi kufanyia kazi mawazo yake sawasawa kwa maana akili haiwezi kuamua kile kinachotoka kwenye ufahamu wake... akisikia piga kelele atapiga, akisikia lia atalia.
Katika roho tunaratibu yote tufahamuyo kwa namna ya imani.
Katika roho tunasikia, tunaona, tunahisi... haya mambo ili yaweze kuleta maana kamili kwa mtoto wa Mungu *ni lazima Imani itafsiri...* na Imani ndio inadhibitisha kwa uhakika kuwa bahari imechafuka lakini Yesu yupo atakusaidia.
Akili hutusaidia kuratibu matendo ya nje... (kupitisha wazo sahihi)
Imani hutusaidia kuratibu matendo ya rohoni (kupitisha taraja)
Ili tuweze kuishi maisha ya rohoni tunahitaji imani na ili imani yetu iwe na nguvu tunahitaji kuwa na Ukweli wa kutosha, taarifa sahihi yaani Neno la Mungu kwa wingi.
.
.
*MAMBO MBALIMBALI UNAYOTAKIWA KUFAHAMU UKIAMUA KUISHI MAISHA YA KIROHO.*
1. Shetani ni muongo.
2. Shetani anamuogopa mtu mwenye Imani ndio maana hupitisha neno la hofu ili apitishe mambo yake.
3. *Yakobo 4:7*
Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.
4. Maamuzi sahihi na ya kweli ndio mwanzo wa ushindi wa kiroho.
5. Majibu yatokayo rohoni ni roho. (Hakuna giza litaweza kupambana na majibu hayo)
6. *Yohana 3:6*
Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.
7. Dhambi uharibu ufahamu. (Ile namna ya kutafsiri mambo ya rohoni)
8. Shetani hana nguvu dhidi yangu nje ya dhambi.
9. Ukiuamini uongo utaongozwa na uongo.
10. Hakuna mafanikio nje ya Kweli (NENO)
11. Mungu ananibadilisha kwa kutumia Neno lake na si mawazo yangu.
12. Hakuna badiliko la KiMungu nje ya Neno la Mungu.
13. Ukweli haumchanganyi mtu, lakini afuataye mambo ya mwilini atajichanganya.
14. Imani ni kupokea na kufanyia kazi vitu ambavyo havieleweki katika akili.
15. Utumishi wako utaanza siku utakayoanza kumsikiliza Mungu, nje ya hapo unajitumikia.
16. Kila kilicho dhahiri mwilini kilianzia katika roho.
17. Ushindi wetu unaanzia rohoni na si mwilini.
18. Rohoni ndio kuna majibu sahihi ya mtoto wa Mungu, na kwa imani atapokea.
19. Mizaha hupunguza au huondoa mamlaka uliyonayo, acha mizaha ili neno lako liwe na nguvu kwenye moyo wa mtu.
20. Kutokupenda kuomba ni kumuambia Mungu unaweza kujitegemea mwenyewe.
21. Kama vile chuma kikikaa nje ya mashine hupata kutu, basi thamani ya mtu ipo ndani ya Kristo.
Yapo mambo mengi sanasana... lakini maisha ya rohoni si jambo la option kwa mtoto wa Mungu.
Mungu alituzaa rohoni ili tuishi katika namna ambayo tutamuelewa... ili maelekezo yake yawe mepesi kutekelezeka.
*Mambo ya Mungu ni magumu sana kama tutaamua kuyatimiza wakati hatujaachana na mambo ya mwilini.*
Previous
Next Post »