TUSIHUBIRI INJILI KWA HASIRA

 

Mungu mwenyewe aliichukia dhambi lakini hajawahi kutumia ukali kuiondoa dhambi. Kwa upendo alimtoa Yesu ili aziondoe dhambi zetu. Ikiwa Mungu hakutuonesha hasira kwanini sisi kuwakasirikia watenda dhambi na kutumia ukali ili kuwarejesha karibu naye? Je ukali una nguvu kubwa ya kuwaleta wengine  kwa Yesu kuliko Upendo?. Tuhubiri injili  kwa moyo wa Furaha, katika tabasamu la sura maana injili ni habari njema. Hakuna Mtu anampelekea mtu habari njema akiwa amekunja sura. Kuchukia dhambi kusikupelekee kuwachukia wenye dhambi. Kama sisi tulipendwa hata tukiwa wadhambi, tunatakiwa kuwapenda wengine,  kuchukuliana nao huku tukiwaonya kwa  Upendo.

ConversionConversion EmoticonEmoticon

:)
:(
=(
^_^
:D
=D
=)D
|o|
@@,
;)
:-bd
:-d
:p
:ng